KERO Baadhi ya huduma za Hospitali Mnazi Mmoja Dar ni kero kwa wananchi

KERO Baadhi ya huduma za Hospitali Mnazi Mmoja Dar ni kero kwa wananchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
4,800
Reaction score
4,859
Hii hospitali ya Mnazi Mmoja ina umuhimu mkubwa sana jijini hasa kwa wananchi wa chini. Jamani uongozi mjitathmini.

Watumishi wengi mno ni kama mko pale kupoteza muda.

1. Huduma ya madaktari ni ya ovyo mno sometimes mnavuruga utaratibu mgonjwa amepanga foleni , pamoja na kujizungusha zungusha na kupotea mkiwaacha muda mrefu wakiwasubiri si ajabu ukawa unasikilizwa halafu daktari mwenzake anaingia na customer wake anakwambia usubiri, mna vijana na mabinti hapo simetimes ni kero tupu, mnachat huku mko na customers just try to be professional.

2 . Hapo x ray ni yale yale mnasubirisha sana watu bila sababu . Watu wanaumia mno kusuniri huduma yenu . Mteja unakaa kwenye foleni sana halafu ukiingia unamkuta msoma x ray yuko on u tube huku mnapiga tu mastory. Hamko professional hata kidogo. You tube kwenye display monitor ya wateja ? Binafsi sikuamini nilichokiona.

3 . Hao wamama watatu kwenye reception kauli zao utadhani magangwe ni shida tupu . Mbaya zaidi wanajua kuwa malalamiko ni mengi sana sasa ukisikia wanavyokoleza inatia hasira. Ukiuliza wanasema wanalalamika na kwenda tena wanakuuliza we unaweza? Dah bongo ni bongo huu upuuzi hata kenya huukuti .

4 Canteen sina jinsi ya kupaelezea maana kiongozi aliyeweka huyo mama ntiliye ambaye nahsi mtaji wake haufiki hata laki mbili kuhudumia madaktri , manesi wafanyakazi wengine na wagonjwa kama ni mimi nina mamlaka hilo tu lingemtoa nje ya kazi . Jamani watanzania tuna matatizo makubwa . Before alikuwepo mtoa huduma makini sana kila kitu kilikuwepo sasa hivi ni aibu aibu aibu . Sehemu very very potential ila mama ntiliye hata soda hana za kutosha na zilizopo unamuta za moto . Mtu mwenye kichefu chefu huwezi kula pale .

4. Kuna discrepancy ya dawa between pharmacists na madaktari. Sometimes.

Shukrani zangu ziende tu kwa viongozi wa huduma ya maternity . Ki ukweli sina la kukosoa mnajituma mno hasa kijana mmoja anaitwa George .yuko na wito kijana na atafika mbali sana . Serikali inajenga mijengo nchi nzima ila hamdeserve kuwa mnatundishia akina mama kwenye hilo banda lina joto sijui degree 40 na hakuna fern.

Otherwise huduma yenu inafuatwa na viunga vyote vya dar. Serikali iwaongeze tu miundombinu na masilahi. Mko wabinifu kufundisha na kuwapigia simu sometimes wamama wajawazito . Mnaangushwa tu na majirani zenu wa pale main hospital out patients ambayo inategemewa na wananchi wengi sana wa hapo dar es salaam hasa wasiokuwa na uwezo .

Toeni huduma makini ndo maana mko hapo mbona awamu ile mlikimbizana kama kuku . Nisimamieni muwape huduma hao watu wasio na uwezo .

Inauma.
 
Nimefika hospitali ya wilaya saa 3, mtu wa x-ray hajafika, akaja kufika nusu saa mbele, kibaya zaidi akakaa kuongea na simu karibia dk 20 kisha ndio anakuja kuuliza shida yetu nini..

Uwajibikaji ni tatizo kubwa saana, system iko corrupted, hakuna uafadhali.
 
Kuna mambo mengi sana nilikua napingana na Magufuli ila vile alivyokuwa anawaongoza Watanzania ndio namna mzuri ya kudili nao. Mtanzania kama ling'ombe hadi ulipelekeshe ndio kazi itafanyika. Bila vitisho vya ntakufukuza kazi, au kumsimamisha anajisahau sana.

Wazee tutengeneze Taasisi imara mambo ya show ya mtu mmoja madhara yake ndio haya.
 
Samia ako na said katika cheka Tu .

Next week katika cheka Tu nadhani episode itakuwa "asante mama Kwa kunipa no, yako 😎
 
Samia ako na said katika cheka Tu .

Next week katika cheka Tu nadhani episode itakuwa "asante mama Kwa kunipa no, yako 😎
Watanzania hawasemi ila awamu hii taasisi ni zinafanya hovyo hovyo hovyo nafuu wangedeal na hospitali tu mengine wakaacha
 
Hivi ni Sahihi kusema Watanzania ni "Wapole" au "Wajinga "??
 
Mama mjamzito anaomba msaada wa kujifungua, nurse anaongea na simu na bwana wa kizigua
 
Ukija moshi huku ndiyo utajuta kuugua. Iwe ni hospitali ya serikali ya dini au mtu bonafsi mateso ni yale yale.
Nilienda st joseph ili kupima mkojo nikaambiwa lazima ulipe 10k ili nimuone daktari aniandikie.
Kumuona daktari, kupima vipimo vingi kumuona daktari tena.-ambaye siyo yule kwanza ilichukua saa 10.
Nilizira matibabu. Nikaondoka zangu saa 3 usiku.
 
Ukija moshi huku ndiyo utajuta kuugua. Iwe ni hospitali ya serikali ya dini au mtu bonafsi mateso ni yale yale.
Nilienda st joseph ili kupima mkojo nikaambiwa lazima ulipe 10k ili nimuone daktari aniandikie.
Kumuona daktari, kupima vipimo vingi kumuona daktari tena.-ambaye siyo yule kwanza ilichukua saa 10.
Nilizira matibabu. Nikaondoka zangu saa 3 usiku.
Mkuu huduma ninzimefifia,
Na kufifia na kufifia , mbaya zaidi watumishi ni corrupt utadhani tupo sudani
 
Back
Top Bottom