KERO Baadhi ya Mabasi ya Mikoani yanasimama sehemu zisizosalama wakati wa 'kuchimba dawa'

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kutoa changamoto yangu kwa Wahudumu wa mabasi hasa ya mikoani, kuna baadhi ya sehemu za mapumziko mafupi kwa ajili ya Watu kujisaidia maarufu kama “chimba dawa” mabasi yao yamekuwa yakiingia sehemu ambazo usalama wa mizigo ni mdogo ndani ya mabasi.

Kwani maeneo mengi kuna wezi ambao abiria wakishuka kwenda kujisaidia au kuchukua vyakula watu hao hujifanya abiria na kupanda haraka kwenye basi then kuiba.

Pia, sehemu hizi za chimba dawa zina sifa moja wapo ya kuwa hazina control ya watu wanaofanya biashara pale na pia mwanga hafifu unaowapa wezi hao uhalali wa kufanya azima yao.

Mie ni mhanga wa hayo matukio, halafu ukiwaambia wamiliki wa mabasi wanakuambia mizigo ya ndani siyo dhamana yao na matukio haya mengi yapo sana mkoa wa Morogoro.
 
Naomba kutoa changamoto yangu kwa Wahudumu wa mabasi hasa ya mikoani, kuna baadhi ya sehemu za mapumziko maarufu kama “chimba dawa” mabasi yao yamekuwa yakiingia sehemu ambazo usalama wa mizigo ni mdogo ndani ya mabasi.

Kwani maeneo mengi kuna wezi ambao abiria wakishuka kwenda kujisaidia au kuchukua vyakula watu hao hujifanya abiria na kupanda haraka kwenye basi then kuiba.

Pia, sehemu hizi za chimba dawa zina sifa moja wapo ya kuwa hazina control ya watu wanaofanya biashara pale na pia mwanga hafifu unaowapa wezi hao uhalali wa kufanya azima yao.

Mie ni mhanga wa hayo matukio, halafu ukiwaambia wamiliki wa mabasi wanakuambia mizigo ya ndani siyo dhamana yao na matukio haya mengi yapo sana mkoa wa Morogoro.
Hamna shukran nyie viumbe weusi
 
We Anonymous si andika bus x lilisimama sehemu flani tunavyotoka A kwenda B siku fulani.
 
Back
Top Bottom