GE2025 Baadhi ya madereva wa bodaboda na vijana wa Mbeya wakataa kuandamana

GE2025 Baadhi ya madereva wa bodaboda na vijana wa Mbeya wakataa kuandamana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wananchi wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wamesema kuwa hawawezi kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria za nchi zenye viashiria vya kuondoa amani ikiwemo maandamano yasiyo na kibali yanayoweza kusababisha vita ambazo zinaendelea baadhi ya Nchi duniani na kuathiri shughuli za kiuchumi ,kukosekana kwa amani na utulivu huku watu wakipoteza maisha kwa kuuana ,njaa na wengine kuishi maisha ya kuhamahama kama wanyama.

Wananchi wilaya ya Rungwe kutoka makundi mbalimbali ikiwemo bodaboda ,wakulima na wafanyabiashara wadogo na wakubwa wametoa msimamo huo baada ya Mbunge mteule wa viti maalum Mkoa wa Mbeya Mh.Suma Fyandomo ambaye amefunga kampeni kwa kutembelea makundi mbalimbali huku akiomba kura za wagombea wa chama chake cha Mapinduzi (CCM) na kutoa elimu ya athari za kutoweka kwa amani kwenye nchi.
 
Back
Top Bottom