Madereva wa Bolt wanakera sana. Unakuta kwenye app imeonyesha nalipa shilingi 3,000, lakini dereva anasisitiza nimlipe 4,000 akidai mara nyingine app ya Bolt huwa inasumbua. Nilimwambia aendelee kumaliza safari (end ride) kwanza, lakini akadai mtandao unasumbua.
Nilipomwambia nitampa hiyo hela anayotaka, lakini amalize safari kwanza, ndipo akaweza kufanya hivyo. Hata hivyo, nilimwambia nitamrekodi na nitamripoti.
Nimeshawasilisha malalamiko kupitia app ya Bolt, lakini hadi sasa wako kimya. Hii inatufanya tupoteze imani na huduma yao. Inasikitisha zaidi kwamba baadhi ya hawa madereva wanakuwa wakorofi unapokataa kuwapa hiyo hela ya ziada.