Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Viongozi wa matawi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kata ya Kunduchi Wilayani Kinondoni wamefika katika ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa kile walichodai kukatwa kwa jina la mtiania wa kata hiyo, Michael Urio.
Hata hivyo majina ya watiania ya udiwani ambayo yalipita kamati za siasa ngazi ya kata wilaya, mkoa na Taifa yamerudi, huku jina la Urio ambaye ni Naibu Meya wa Kinondoni likikosekana.
Majina yaliyorudi walioteuliwa ni Emmanuel Mkuchu, Happiness Kinyaha na Joyce Haule.
Kundi hilo lililofika saa tatu asubuhi katika ofisi hizo za mkoa kwaajili ya kukutana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu waliingia ofisini kukutana naye saa nane mchana.
Baada ya kikao cha karibu saa zima ambacho waandishi waliambiwa wasubiri nje, wanachama baada ya kuongea na Mwenyekiti huyo ambaye ndiye mlezi wa chama wakatoka nje.
Wakielezea kilichotokea na majibu waliyopewa kwenye kikao hicho kwanza wamesema wamesikitishwa na kitendo cha kukatwa kwajina la mtiania huyo ambaye ameiongoza kata ya Kunduchi kwa miaka 10.
Hata hivyo, wameridhia uamuzi waliofikia ndani ya kikao walichoketi na Mwenyekiti Mtemvu ya kwamba wasiwe na wasiwasi ila wangoje vikao vya siasa vitakavyoketi kesho na keshokutwa kisha hadi Agosti 2, 2025 kutakuwa na majibu ya kile kilichotokea.
Chanzo: Mwananchi