Baadhi ya makosa ambayo enzi zetu ulikuwa ukifanya unagongwa bakora za kukutosha

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Watoto wa zamani ulikuwa ukifanya makosa yafuatayo ulikuwa unalamba bakora za kutosha

1. Usiposalimia wakubwa asubuhi, unapigwa.
2. Usiposalimia wageni, unapigwa.
3. Ukinawa kabla ya wageni, unapigwa.
4. Ukilia bila sababu, unapigwa.
5. Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka, unapigwa.

6. Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni, unapigwa.
7. Ukikaa wakubwa wamesimama, unapigwa.
8. Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi, unapigwa.
9. Ukichelewa kurudi toka shuleni, unapigwa.
10. Ukiwahi kurudi shuleni, unapigwa.

11. Ukililia wageni wakati wanaondoka wakitoka, unapigwa.
12. Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula, unapigwa.
13. Kujibu ovyo wakubwa, unapigwa.
14. Kutukana watu wazima, watoto au rika lako, unapigwa.
15. Ukiwa mbishi bila sababu, unapigwa.

16. Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze.
17. Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie.
18. Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa.
19. Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa, unapigwa.
20. Ukila kwa jirani ukabainika, unapigwa.

21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani, unapigwa.
22. Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa, unapigwa.
23. Ukimkuta mtu nzima hujampokea, unapigwa.
24. Ukienda kusema kama umepigwa, unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia, unapigwa.

26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani, unapigwa.
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani, unapigwa.
28. Ukianza kuchaguwa chakula hiki nakula hiki sili, unapigwa.
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao, unapigwa.
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli, unapigwa.

31. Ukikaa na wakubwa halafu ukaanza kucheka bila sababu, unapigwa.
32. Ukimwuliza Baba/ Mama umetoka wapi unapigwa.
33. Ukilala bila kula, unapigwa.
34. Ukiitwa ukaja kimyakimya bila ya kuanza kuitika unapigwa.
35. Endapo umepigwa na ukasusa chakula, unapigwa.

Sasa hiki kizazi cha sasa cha kunyoa viduku, wanawake kuvaa suruali, wanaume kusuka na kuvaa heleni, kizazi cha kusagana na ushoga, kuvalia suruali chini ya matako, nk hawayajui haya. Eti sasa hivi ukimgombeza tu mtoto anatoroka nyumbani, ukimpiga anakwenda ustawi wa jamii
 
Pole sana ndg yetu! Umepitia wakati mgumu sana! Kuna wazazi/walezi huamini fimbo ndio kila kitu kwenye malezi. Wanashindwa kutambua kwamba wakati mtoto hayo ni makuzi tu, na anaweza kuonywa na akabadilika pasipo viboko.

Mfano kuna baadhi tuliadhibiwa kwa kuimba nyimbo ambazo hazikuwa na maadili pasipo kujua maana! Tofauti na zama za leo watoto wanaiga nyimbo za wasanii zisizo maadili na zinaimbwa na watu wazima! Utamsikia mtoto yuko busy anaimba "basi ntongozeee"
Duh! Mambo yamebadilika sana!
 
Wakina junior siku hizi ata kusalimia hawasalimii aisee inakukodolea macho tu na wazazi utawasikia uyo ndo alivyoo😀😀
 
Majunia wa Dar labda.
Mikoani mbona vitoto vinasalimia?
Tena huku Kaskazini unapishana na katoto, hukajui hujawahi kukaona lkn kanasalimia.
 
Pole sana ndg yetu! Umepitia wakati mgumu sana! Kuna wazazi/walezi huamini fimbo ndio kila kitu kwenye malezi. Wanashindwa kutambua kwamba wakati mtoto hayo ni makuzi tu, na anaweza kuonywa na akabadilika pasipo viboko.

Mfano kuna baadhi tuliadhibiwa kwa kuimba nyimbo ambazo hazikuwa na maadili pasipo kujua maana! Tofauti na zama za leo watoto wanaiga nyimbo za wasanii zisizo maadili na zinaimbwa na watu wazima! Utamsikia mtoto yuko busy anaimba "basi ntongozeee"
Duh! Mambo yamebadilika sana!
Ila ukweli unabaki kuwa bakora ndiyo adhabu pekee mtu anaweza kujutia kosa lake. Sababu adhabu ni shariti itoe maumivu kwa mtenda ili liwe funzo kwake ili asirudie kosa. Ndo maana kuna kifungo, voboko, nk
 
Majunia wa Dar labda.
Mikoani mbona vitoto vinasalimia?
Tena huku Kaskazini unapishana na katoto, hukajui hujawahi kukaona lkn kanasalimia.
Chugga kweli vina heshima ila uku Dar na Moro ni balaa😀😀
 
Cha kufurahisha zaidi, ulikuwa ukitumwa kwa jirani, ukikuta wanakula wakikukaribisha kula ukakataa, watakuambia subiri tumalize kula ndo utapewa ulichotumwa. Wakimaliza kula tu unagongwa bakora za maan ndo unapewa ulichotumwa na unaondoka na mtu kwenda nyumbani kwenu ili kukusemelea kuwa umekataa kula. Huko nyumbani tena unagongwa nyingine kwa kukataa kula. Yani ilikuwa full respect, binti anafika miaka 20+ lakini akikutana na mwanaume njiani either atabadilisha njia au atamkimbia ili asitongozwe. Enzi hizo mabikira walikuwa siyo wa kuhesabu, walijaa tele.
 
1. Usiposalimia wakubwa asubuhi, unapigwa.
2. Usiposalimia wageni, unapigwa.
3. Ukinawa kabla ya wageni, unapigwa.
4. Ukilia bila sababu, unapigwa.
5. Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka, unapigwa.
6. Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni, unapigwa.
7. Ukikaa wakubwa wamesimama, unapigwa.
8. Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi, unapigwa.
9. Ukichelewa kurudi toka shuleni, unapigwa.
10. Ukiwahi kurudi shuleni, unapigwa.
11. Ukililia wageni wakati wanaondoka wakitoka, unapigwa.
12. Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula, unapigwa.
13. Kujibu ovyo wakubwa, unapigwa.
14. Kutukana watu wazima, watoto au rika lako, unapigwa.
15. Ukiwa mbishi bila sababu, unapigwa.
16. Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze.
17. Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie.
18. Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa.
19. Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa, unapigwa.
20. Ukila kwa jirani ukabainika, unapigwa.
21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani, unapigwa.
22. Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa, unapigwa.
23. Ukimkuta mtu nzima hujampokea, unapigwa.
24. Ukienda kusema kama umepigwa, unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia, unapigwa.
26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani, unapigwa.
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani, unapigwa.
28. Ukianza kuchaguwa chakula hiki nakula hiki sili, unapigwa.
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao, unapigwa.
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli, unapigwa.
31. Ukikaa na wakubwa halafu ukaanza kucheka bila sababu, unapigwa.
32. Ukimwuliza Baba/ Mama umetoka wapi unapigwa.
33. Ukilala bila kula, unapigwa.
34. Ukiitwa ukaja kimyakimya bila ya kuanza kuitika unapigwa.
35. Endapo umepigwa na ukasusa chakula, unapigwa.
Wahenga njooni tukumbushane matukio mengine
 
Mdogo wako akipigwa na wewe upo mkirudi nyumbani utapigwa
 
Back
Top Bottom