Baadhi ya makosa ambayo enzi zetu ulikuwa ukifanya unagongwa bakora za kukutosha

Hizi ndio kali zaidi

16. Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze.
17. Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie.
 
No. 14 siyo tu kupigwa unawekwa kikao cha ukoo kabisa πŸ˜‚
 
Usipolima kwa spidi shambani siku hiyo hautakula na usipokula utapigwa kwanini haukula

Kama mna mifugo usipoenda machungani utapigwa
 
Nasoma naona kama umeandika yote. Ila watoto wa zamani tulinyooka kitabia. Shuleni kwenyewe ukiwa mtovu wa nidhamu walimu wakakubaini utaishia kuandikwa kwenye kitabu cheusi, black book na ukifaulu huendi sekondari hata kama una akili nyingi. Sasa hivi ukiadhibu mtoto wa mtu kwa utovu wa nidhamu utajikuta matatani huko polisi. Zamani mtoto alikuwa ni wa jamii nzima, sio wa serikali pekee kama ilivyo sasa. Serikali inajifanya kulinda haki za watoto huku ikishindwa kulinda mmomonyoko wa maadili kwa watoto wanakua wakiwa wakubwa na tabia za kishenzi zisizopendeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…