Possibles
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 1,943
- 2,482
MKUKUTA, MKURABITA, Reforms za TAMISEMI maana kabla ya hapo mfumo wake ulikuwa haujakaa vizuri.
Lakini kama kuna mambo niliyafurahia wakati wa utawala wake basi ni haya:
1. Kudhibiti mfumuko wa bei. HApa sijui alifanyaje. Kwa miaka 10 bei ya bidhaa ilikuwa ya kawaida mno. Ukiwa na elfu moja una uwezo wa kununua soda 5 hadi 6 kwa wageni wako.
2. Uwezo wake mkubwa aliyouonesha katika kushiriki mijadala ya kimataifa na mahojiano ya mashirika makubwa ya habari haswa akiwa nje ya nchi. Alijiamini mno.
3. Mfululizo wa hotuba zake za kila mwezi. Nilivutiwa sana na hotuba zake. Alieleza mambo mengi hadi ziara zake nje ya nchi alisema dhumuni, kilichotokea na faida ya ziara husika kwa Taifa. Nakumbuka nilikuwa nikikuta hotuba yake inarushwa nitaisikiliza mpaka mwisho.
KILICHONISHANGAZA: Sijawahi kumsikia akitania au akifanya utani tofauti kabisa na watu wengi wa kusini. Alikuwa 'a serious and no nonsense man'.
Mwenyezi MUNGU amlaze mahali pema peponi.