Baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye ajira za ualimu 2021

Baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye ajira za ualimu 2021

Kumbuka kuhusu five six kwa mwaka mmoja
Ujue unazungumza na watu wazima humu kwahiyo usifikiri kwamba sisi ni watoto unaoweza kuwadanganya kirahisi na kadri utakavyowakingia kifua ndio utawaharibia zaidi kwa sababu hao madogo wamehitimu bachelor degree mwaka jana na taarifa zao zipo
 
Waziri hana jipya, bila kuhonga hapa hakuna kupata kazi. Nawaonea huruma wadogo zetu mtaani.
Afu mtu anajitapa et mimi nisingetoa pesa mke wangu asingepata kazi.
 
Pamoja na kujitutumua ila naona hii wizara ni kubwa kuliko waziri mwenye dhamana nayo,time will tell...
 
Mkaruka nadhani bado hujaelewa hoja yangu ni hivi kwa mwanafunzi aliyemaliza form four 2014 kama alienda direct ilibidi digrii yake ya kwanza ya ualimu aipate 2020 lakini wao inaonyesha wameipata 2019. Je ni chuo gani kinachotoa shahada ya ualimu kwa miaka miwili???
Mdau mmoja katoboa siri hapo juu kuwa hao walimaliza mwaka jana 2020 walipoona vigezo ni waliomaliza 2019 wakaomba hivyohivyo kwa kuandika 2019
 
Uchambuzi wako ni mzuri sema umejisahau kwamba wengine wanasoma kidato cha sita kwa mwaka mmoja hawaendi ni hizo nakba zako za miaka 2,zingatia hilo hil,anaweaa kuwa alimaliza 2014 kidato cha 4 ila akafanya mtihani kama PC kw mmoja mbele akatoboa akazama chuo......usikariri mkuu
 
Mnapotoa kasoro mkumbuke mambo mawili

Moja Kuna mtihani unaitwa qt five six kwa mwaka mmoja

Pili kuna mtu kupata zero na akareset mtihani

Mimi naona ha jalifikilia hilo
Yeye naona amekariri hajui kwamba kuna wanao risit na wale wanaofanya QT
 
Waziri hana jipya, bila kuhonga hapa hakuna kupata kazi. Nawaonea huruma wadogo zetu mtaani.
Afu mtu anajitapa et mimi nisingetoa pesa mke wangu asingepata kazi.
Duh sio tu anajioshea kwa mamaa wife wewe umemuamini kweli
 
Yeye naona amekariri hajui kwamba kuna wanao risit na wale wanaofanya QT
Yuko sahihi ila wewe ndiye umekariri mkuu. Wanao reseat na QT registration number zao zinaanza na herufi(P) kuashiria private candidate kwa maana hiyo hao walimu wamesoma katika mfumo wa direct (formal education) ndio maana registration number zao zimeanza na herufi S.
 
Pamoja na kujitutumua ila naona hii wizara ni kubwa kuliko waziri mwenye dhamana nayo,time will tell...
Muda mwingine unaweza kumlaumu waziri bila kujua ugumu na uzito wa wizara anayoiongoza. Mimi nilikuwa nashauri ili kurahisisha utendaji kazi hii wizara ingepunguziwa mzigo mfano masuala ya elimu yangerudishwa kwenye wizara ya elimu na Tamisemi ikabaki chini ya ofisi ya wizara mkuu kama zamani
 
Aina hii ya makosa imezoeleka sasa. Hata ajira za mwaka jana ( 2019) kasoro za aina hii zilijitokeza lakini hawakujitokeza kutoa ufafanuzi walakujulisha Watanzania hatua walizochukua juu ya kasoro hizo
 
Mwingine huyoo!
FB_IMG_16249041868171901.jpg
 
Back
Top Bottom