Kikosi cha Yanga kwa kundi la pili limepaa leo alifajiri kuifuata CBE SA ya Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wachezaji walioondoka leo ni wale ambao walikuwa hawana majukumu kwenye timu zao za taifa, wakati mastaa kama Djigui Diarra, Prince Dube, Duke Abuya na Khalid Aucho waliripotiwa kutua nchini Ethiopia jana.
Clatous Chama pamoja na Kennedy Musonda wanatarajiwa kufika nchini humo leo wakiwa wanaungana na wachezaji wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kilichocheza mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Guinea juzi na kushinda mabao 2-1.