KWELI Baadhi ya njia za asili za uzazi wa Mpango si salama

KWELI Baadhi ya njia za asili za uzazi wa Mpango si salama

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #2
View Source #2
Mfano matumizi ya majivu kuchanganya na maji ya uvuguvugu na kunywa masaa 2 kabla ya tendo pamoja na njia nyingine ni matumizi ya unga wa mbegu za papai, ni salama kiasi gani?

pJBktkpTURBXy8wYjAxYTY0M2ZiMTc1MDc1NjEwYmNjOTRjNWVhMTU2ZC5qcGeSlQMAB80C980BqpMFzQKAzQFA.jpg
 
Tunachokijua
Mbegu za papai (Carica papaya) hutajwa kuwa na uwezo wa kuathiri mfumo wa uzazi kwa jinsia zote mbili. Kwa wanaume, hupunguza uzalishwaji wa mbegu za kiume Pamoja na kuathiri kasi na maumbo yake. Kwa wanawake, baadhi huzitumia kama njia ya kiasili ya uzazi wa mpango. Haya yanathibitishwa na Utafiti wa AE Memudu (2021) na V. Ghaffarilaleh et al (2019)

Mwaka 2000, N K Lohiya kutoka Chuo Kikuu cha Rajasthan, India, kwenye mkutano unaoangazia masuala ya changamoto zinazokabili afya uzazi nyakati hizi alitangaza kuwa kampaundi 4 alizozichakata kutoka kwenye mbegu za papai zinaweza kutoa majibu chanya kwenye kuthibiti uzazi. Utafiti huu unajenga msingi wa matumizi ya mbegu za mapapai kama njia ya asili ya uzazi wa mpango.

Matumizi ya majivu kama njia ya asili ya uzazi wa mpango bado haijathibitishwa kisayansi, ni tendo linalofanyika mitaani likiwa na msingi wa Imani za kale ambazo hazina mashiko kisayansi.

Kwa kiasi kikubwa, majivu huundwa kwa carbon pamoja na kiasi kidogo cha Madini ya calcium, magnesium, potassium na phosphorus. Huwa pia na kemikali zinazoweza kuathiri mwili kwa kusababisha magonjwa sugu hasa saratani. Hadi sasa, hakuna tafiti za kisayansi zinazothibitisha ufanisi wa majivu kwenye kuzuia ujauzito.

Pamoja na ukweli kuwa njia hizi zimetumika kwa muda mrefu, kiwango cha ufanisi wake Pamoja na madhara tarajiwa ya muda mfupi na muda mrefu hayajulikani. Ni bidhaa zisizo chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Dawa na Chakula ya Marekani (FDA) na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Pia soma:
Njia za Asili za Uzazi wa Mpango (Natural birth control methods)

Kwa kuzingatia kemikali mbalimbali zinazopatikana kwenye majivu na Mbegu za papai ambazo siyo zote ni salama kwa afya, Pamoja na kukosekana kwa mchakato wa kisayansi unaoweka udhibiti wa uzalishaji na upimaji wa madhara ya dawa na chakula, njia hizi zinaweza zisiwe na ufanisi wa mkubwa, pia usalama wa kutosha.

United Nations Population Fund (UNFPA) wanaonya matumizi ya njia hizi kwa kuziita kuwa “Ni njia zisizo salama na haziaminiki” hivyo watu wanapaswa kuziepuka.

Baadhi ya njia za uhakika za kiasili za kupanga uzazi zinazoweza kutumika pasipo kumuathiri mama ni kalenda au matumizi ya vifaa vinayofuatilia mzunguko wa hedhi ya mwanamke, kumwaga nje shahawa wakati wa tendo la ndoa Pamoja na kunyonyeza mfululizo ndani ya miezi 6 ya mwanzo baada ya kujifungua.
Back
Top Bottom