A
Anonymous
Guest
Baadhi ya polisi wa barabarani wamekuwa wakiandikia fine malori ya mizigo kwa makosa ambayo hayapo ili wajipatie pesa. Mfano kosa la gari bovu. Gari limetembea kutoka Mwanza hadi Dar ila wanasimamisha wanaandika gari bovu kisa hamna nati moja au mbili au bumber limechomoka.
Gari bovu linawezaje kutembea barabarani na kama ni bovu ziwekwe sheria magari mabovu yasiwepo.
Pili kuna fine ya "defective tyres" yani tairi mbovu. Lorry lina tyre kuanzia 10 mpaka 22. Wakikuta tairi 1 au 2 zimeanza kuchoka wanakupiga fine. Sasa najiuliza kwa biashara gani kila siku utanunua tyre nzima!
Njia zenyewe ni mbovu sana ndio maana magari yanachoka na bado ukifika barabara kuu unapigwa fine. Polisi wenyewe ukiangalia magari yao ya kazi au binafsi yamechoka sana ila kutwa wanapiga fine magari mengine.
Huu ni uonevu sana na wanafanya biashara za watu ziwe ngumu sana.
Na polisi ukimuuliza kwanini unapiga fine wakati gari liko sawa anajibu tumepewa target ya makusanyo.