Baadhi ya sababu za kuinyima kura Serikali ya CCM Oktoba 2020

Baadhi ya sababu za kuinyima kura Serikali ya CCM Oktoba 2020

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
5,146
Reaction score
15,927
Kuelekea uchaguzi mkuu 2020, ndugu mtanzani amini usiamini unao uwezo wa kuiondoa CCM madarakani, nitaelezea kwenye uzi mwingine jinsi unavyoweza kulitumia sanduku la kura kuleta mageuzi chanya. Kwa leo naomba tukumbushane machache tu ambayo serikali ya CCM imeyafanya na hivyo kustahili kupewa mkono wa kwaheri hiyo October.

Wafanyakazi.
1. Kikokotoo cha mafao (bado kipo, mwenyekiti ameamua kukiondoa kwa muda ili watu wasahau kidogo)
2. Kuunganishwa mifuko ya hifadhi ya jamii (wastaafu wanakiona cha mtema kuni, haikuunganishwa kwa ajili ya maslahi za wafanyakazi)
3. Bodi ya mikopo (makato ya 15% kila mwezi + riba ya 6% kila mwaka)
4. Mkwamo wa kupanda vyeo makazini
5. Kupoteza ajira (hususani wafanyakazi wa sekta binafsi)

Wafanyabiashara.
1. Utitiri wa kodi na tozo kandamizi
2. Kupungua kwa uwezo wa kununua bidhaa kutokana na vipato vya watu kushuka

Wakulima.
1. Serikali kuvuruga masoko ya mazao ya kilimo
2. Serikali kuikacha sera ya kilimo kwanza, hakuna cha mbolea ya ruzuku wa nini


Watanzania kwa ujumla
1. Ukatili uliokithiri wa vyombo vya dola (watu wanauawa kwenye vituo vya polisi mpaka ndugu wanagoma kuchukua maiti za wapendwa wao n.k)
2. Udikteta na kutotaka kuwajibishwa kwa viongozi wa CCM (wamejiongezea na kinga hivi majuzi ili wawe na uhuru zaidi wa kuvunja katiba )
3. Kuminywa kwa uhuru wa watu kutoa maoni yao na vyombo vya habari (ukitizama taarifa ya habari basi unaweza kuvunja TV yako, ni kisifu na kuabudu 24/7)
4. Uungu mtu wa viongozi wa awamu ya tano (hususani mwenyekiti, si mtumishi wa wananchi tena bali amegeuka kuwa mtawala wa wananchi wanyonge)
5. Utekaji na mauaji holela ya raia yasiyo na majibu (ni wajibu wa kikatiba wa serikali kuhakikisha usalama wa raia na mali zao)
6. Ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma (miradi yenye mkono wa mwenyekiti haikaguliwi, pesa ya umma inateketezwa kwenye miradi ya aibu kama vile kununua midege bila kuwa na business plan yoyote na kujenga airpot ambayo mwaka mzima inatumiwa na abilia mmoja tu, mwenyekiti!)
7. Ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana

Hayo ni machache tu, mengine tunaweza kuendelea kukumbushana, yote hii ni ili kuhakikisha tunafanya uamuzi sahihi octoba.
 
Kampeni za mwaka huu zinaweza kuwa mbaya zaidi kwa CCM tofauti na tunavyozani, Wananchi wana hamu ya kuwasikia Wapinzani wakiongea, CCM kwa miaka mitano wamekuwa wakiongea wao tu, sidhani kama wana jipya.......tusubiri tuone.
 
Kampeni za mwaka huu zinaweza kuwa mbaya zaidi kwa CCM tofauti na tunavyozani, Wananchi wana hamu ya kuwasikia Wapinzani wakiongea, CCM kwa miaka mitano wamekuwa wakiongea wao tu, sidhani kama wana jipya.......tusubiri tuone.
Mambo mengi sana yataibuliwa, na CCM hawatokua na muda wa kuyajibu kwa hoja.
 
1592141599926.png
 
Back
Top Bottom