DOKEZO Responded Baadhi ya Shule za Msingi Wilaya Missenyi-Kagera, Walimu wanawaagiza Wanafunzi vyuma chakavu kwa manufaa yao binafsi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Baadhi ya Walimu katika Shule za Msingi Mugana A na Katarabuga ziliyopo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wanawaagiza Wanafunzi vyuma chakavu ambavyo vimekuwa vikiuzwa kwa ajili ya manufaa yao binafsi kujipatia kipato.

Wanafunzi wakitoka shuleni unaona wanazunguka kwenye mashamba ya watu wakitafuta vyuma chakavu, ukiwauliza wanakwambia wameagizwa shuleni.
photo_2025-06-01_13-18-31.jpg
Lakini kibaya zaidi huu umekuwa kama utaratibu rasmi ambapo mtoto akifeli somo au kufanya kosa anapewa adhabu ya kuleta vyuma chakavu.

Katika mazingira hayo imekuwa ikisababisha Watoto kuchukua vifaa vya ndani na kuvifanya vyuma chakavu pia inaweka Watoto katika mazingira hatarishi wanapokuwa natafuta vyuma chakavu.

Baadhi ya Shule ambazo imebainika wazi kuna utaratibu huo ni Shule ya Msingi Mugana A, Katarabuga lakini nimeelezwa kwamba jambo hili linafanyika hata kwenye Shule nyingine ndani ya Wilaya hiyo.

Nitoe wito kwa Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kufuatilia kwa ukaribu suala hilo na kulipiga marufuku, ikiwezekana wahusika wachukuliwe hatua stahiki.

Majibu ya Halmashauri kuhusu hoja ya Mdau ~ Halmashauri ya Missenyi yasema inachunguza madai ya baadhi ya Walimu Wilayani hapo kuwaagiza Wanafunzi vyuma chakavu

​
 
Duh tabia mbaya sana. Waalimu waache tamaa inawatesa watoto wa watu
 
Hao walimu hawajafanya kosa lolote kwa kuwa wameruhusiwa kula kwa urefu wa kamba zao.
PS
Waone,ukiwa na ushahidi, mmoja wa hawa wafuatao:
Mkurugenzi, mkuu wa wilaya, katibu tawala, au afisa elimu
 
Baadhi ya Walimu katika Shule za Msingi Mugana A na Katarabuga ziliyopo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wanawaagiza Wanafunzi vyuma chakavu ambavyo vimekuwa vikiuzwa kwa ajili ya manufaa yao binafsi kujipatia kipato.

Wanafunzi wakitoka shuleni unaona wanazunguka kwenye mashamba ya watu wakitafuta vyuma chakavu, ukiwauliza wanakwambia wameagizwa shuleni.
Lakini kibaya zaidi huu umekuwa kama utaratibu rasmi ambapo mtoto akifeli somo au kufanya kosa anapewa adhabu ya kuleta vyuma chakavu.

Katika mazingira hayo imekuwa ikisababisha Watoto kuchukua vifaa vya ndani na kuvifanya vyuma chakavu pia inaweka Watoto katika mazingira hatarishi wanapokuwa natafuta vyuma chakavu.

Baadhi ya Shule ambazo imebainika wazi kuna utaratibu huo ni Shule ya Msingi Mugana A, Katarabuga lakini nimeelezwa kwamba jambo hili linafanyika hata kwenye Shule nyingine ndani ya Wilaya hiyo.

Nitoe wito kwa Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kufuatilia kwa ukaribu suala hilo na kulipiga marufuku, ikiwezekana wahusika wachukuliwe hatua stahiki.
Subiria matusi toka kwa walimu wa Jf... Humu walimu ni watakatifu hawasemwi!
 
Mishahara haitoshi! Madeni ya Vikoba na Benk,Sadaka za kausha damu,kodi ya nyumba,karo za watoto,nk
 
Daah kweli watu wamechoka ila ndo hao hao October yanawaumiza watanzania yani mafani mengine michosho tu.
 
Back
Top Bottom