KERO Baadhi ya Shule za Serikali Rombo zinatoza Tsh. 40,000 kusajili Wanafunzi wa Darasa la Kwanza

KERO Baadhi ya Shule za Serikali Rombo zinatoza Tsh. 40,000 kusajili Wanafunzi wa Darasa la Kwanza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero.

Mimi ni mkazi wa Kijiji cha Mengwe, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ninawasilisha kero kwa niaba ya wakazi wenzangu wa Rombo.

Muhula mpya wa Masomo umeanza Januari 13, 2025 lakini kinachoendelea huku Rombo ni wizi mkubwa tena wilaya ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda.

Sisi wazazi wa Wilaya ya Rombo tunawasilisha kero yetu kutokana na Shule za Msingi wilaya ya Rombo Kukataa kupokea wanafunzi wa Darasa la Kwanza hadi ulipie Kiasi cha Shilingi elfu Arobaini.

Shule nyingine ni elfu thelatini na nyingine hadi elfu hamsini.

Wikiendi iliyopita nilimpeleka mtoto shule kwenda kumsajili ila nilishangazwa sana kuambiwa kuwa ni lazima nilipie hiyo Tsh elfu Arobaini ili mtoto asajiliwe.

Wazazi tulihoji hiyo fedha ni ya nini tukaambiwa ni Ya Ulinzi, hata wazazi tulipojaribu Kuomba tulipe kwa awamu walimu walikataa kabisa.

Kulipa hiyo fedha sio tatizo kwetu ila ni vyema serikali iweke utaratibu mzuri na iwaeleze ukweli wazazi ili kujiandaa mapema kuliko kusababisha usumbufu wa iana hii.

Masha ya kijijini elfu arobaini sio hela ndogo kabisa, lakini pia kama sera ya Elimu Bure imeshindikana iondoeni kabisa ili Wazazi tulipie ada na michango mingine bila manunguniko, kujinadi jukwaani elimu bure huku mnachangisha kimyakimya ni kutuona Watanzania ni wajinga.

Naomba Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rombo, Mbunge na Waziri wa Elimu - Mkenda Adolf Muingilie kati na kutolea ufafanuzi jambo hili haraka iwezekanavyo.

Serikali ya CCM iache kuhadaa Wananchi kuwa sera ya elimu bure kuanzia STD 1 HADI Kidato cha sita. Shuleni kuna michango kibao.

Hii ni kero ya sisi wakazi wa Wilaya ya Rombo, kama nawe Mdau kwenye eneo lako kuna kero naomba uwasilishe hapo.

==============================

MKURUGENZI WA ROMBO AELEZA
Akijibu hoja hiyo ya Mwanachama wa JamiiForums, Mkurugenzi Mtendaji wa Rombo, Godwin Justin Chacha amesema:

Suala hilo halijafika mezani kwangu na kwa ufupi fina taarifa kama linafanyika au la, pamoja na hivyo hai wanaolalamika hivyo wasije kuwa wanachanganya michango ya kujitolea ya chakula.

Pamoja na hivyo naomba nilifuatilie kujua suala hilo lipo kweli na kama Wazazi au Walezi hawajafikisha taarifa katika ofisi yangu.
 
Yelewiiii!! Yesuuu na Mariaah! Mankaa! Sisi wachaga tuna helaaa! Sasa nani huyu tena amekuja kutunanga sisi wachaga wa rombo etiii!
 
Kero sana Juzi maam yangu ananipigia Simu Shule ya Msingi Masho ananiambia wamekataa kumpokea mtoto hadi nilipie kiasi cha elfu arobaini yaani ni wapuuzi kweli
 
Kero sana Juzi maam yangu ananipigia Simu Shule ya Msingi Masho ananiambia wamekataa kumpokea mtoto hadi nilipie kiasi cha elfu arobaini yaani ni wapuuzi kweli
Hakuna mchango unaochangishwa bila makubaliano ya wazazi.
Hapo huenda ni hesabu ya chai au uji kwa watoto au hata madawati
 
Jamani nyieee! Sisi wachagga tuna hela mpaka tunaumwa! Kwanza michango yetu ni kuanzia laki mbili na nusu! Sasa huyu ni mchagga wa rombo au muamiaji? Yelewiiii! Yesu na mariah! Tafuta hela I seeee!
 
Sasa elf 40 kitu gani? Hebu tuwe serious.....mambo ya kijinga kama Harusi na saizi kuna upuuzi mpaka besidei mnachanga.....toa hela hiyo.........acha siasa kwa manufaa ya watoto wako
Kweli kabsa. lakini hebu tubaki kwneye hojaya msng kwanini serikali inadanganya elimu ni Bure/ hivi unafikiri watu wanaoishi kijijini elfu arobaini ni hela ndogo? kijijini wanafunzin wanaenda hadi shule na ndala hawana hata elfu tano ya kiatu mkuu.

Tuache ushabiki wa kijinga kwa sababu ya Ubinafsi fikiria hapo kijijni kwenu familia ngapi zina uwezo wa kumudu hiyo gharama? hapo bado uniform madaftari na dawatu ununue mwenyewe
 
Back
Top Bottom