Baadhi ya tuzo za wafanyakazi bora zinafikirisha

Mr. Marangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,574
Reaction score
1,549
Baadhi ya Tuzo zilizotolewa zinafikirisha, kwa mfano mkurugenzi anapokeaje tuzo ilihali katika taasisi anayoiongoza ina watu zaidi ya 100 ambao wao ndio wanaofanya kazi kwa kutaabika kumenyeka, muda mwingine kuhatarisha afya na maisha yao.

Hivyo kwangu mimi kumshindanisha kiongozi wa Taasisi na mtumishi wake haiko sawa, anaefanya kazi sana ni mtumishi, kiongozi ni mchora ramani na muongoza dira.

Nafikiri viongozi wa Taasisi wangekua na tuzo zao ambazo zitashindanisha Taasisi zao mathalani Tuzo za Taasisi zote, tuzo za Taasisi husika Mathalani Viongozi wa Tanesco kwanzia ngazi ya miji mpaka Taifa
Hivyo kwayaliotokea jana nikama Tuzo za mchongo.

Na kwa utafiti kasiko rasmi wale viongozi wakubwa walilamba tuzo zenye mkwanja mrefu.

Tuzo hizi pia zinapaswa kuangaliwa vizuri kwakushindanisha watu wanaofanya kazi zinazo landana, kumshindanisha Daktari na Afisa maendeleo au Afisa nyuiki automatic Daktari ataonekana anapaswa kushinda.
 
Tanzania ndo hii sasa
 
Usimamiz makini wa Mkurugenzi ndio chachu ya wafanyakaz kuwa Bora.

Mkurugenzi mzembe huuwa taasisi lakin mfanyakaz wa Chini akiwa mzembe NI kosa la Mkurugenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…