Baadhi ya vijana vyuoni na wanaoingia vyuoni wanakaubishi fulani fulani kujiona wanajua

Baadhi ya vijana vyuoni na wanaoingia vyuoni wanakaubishi fulani fulani kujiona wanajua

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Hivi vitoto mda mwengine vinakasirisha sana.ukimueleza unatakiwa kupitia hivi basi analeta uchuo uchuo wake unatamani kukazapa vibao.

Vijana wengi waliopo vyuo ndoto zao wanaamini kuajiliwa serikalini ila sio ajira zote zinatoka serikalini.

Vikiwa chuo vinajiona vimetoboa maisha na kutucheka baba na mama zao tuliopo huku mtaani tuna fanana na vyuma chakavu.

Vyengine vinajifanya vitaalamu vya fasihi na uchumi utazani walizaliwa kabla ya wazazi wao.

Sikilizeni wazazi na wakubwa wenu wanajua wanayopitia na wapi pakutokea.

unakakuta kanasoma political science katoto ka mkulima hata baba yake katibu tarafa ajawai shika.

Someni vitu ambavyo vipo kwa ajili ya wazazi wenu kuendeleza kama mmepata bahati ukoo wenu.
 
Vipi hao wazazi mnaoonekana kama vyuma chakavu na nyie hamkuwasikiliza wazazi wenu? Haya maisha siyo ya kupangiana kiivo, ukinishauri inatosha maamuzi yanabaki juu yangu brother kaka.
 
Hivi vitoto mda mwengine vinakasirisha sana.ukimueleza unatakiwa kupitia hivi basi analeta uchuo uchuo wake unatamani kukazapa vibao.

Vijana wengi waliopo vyuo ndoto zao wanaamini kuajiliwa serikalini ila sio ajira zote zinatoka serikalini.

Vikiwa chuo vinajiona vimetoboa maisha na kutucheka baba na mama zao tuliopo huku mtaani tuna fanana na vyuma chakavu.

Vyengine vinajifanya vitaalamu vya fasihi na uchumi utazani walizaliwa kabla ya wazazi wao.

Sikilizeni wazazi na wakubwa wenu wanajua wanayopitia na wapi pakutokea.

unakakuta kanasoma political science katoto ka mkulima hata baba yake katibu tarafa ajawai shika.

Someni vitu ambavyo vipo kwa ajili ya wazazi wenu kuendeleza kama mmepata bahati ukoo wenu.
Hawawezi kukusikia si leo wala kesho .

Maana walimu wa field walipoenda shuleni kwao waliwaambia study hard when you reach university everyrhing will be ok .

Shida ilianzia hapo maana sasa tayari boom wamepata asilimia mia , akiweza kuvaa vizuri kama msomi uchwara kwa suti za karume yaani suruali karume na koti la suti linachukuliwa tandika basi wanahisi maisha tayari .

Hapo bado hajanunua infinix aanze kupiga picha akiwa mkuki house zile siku boom likiingia

Anhaa kaka chizcom kwa saikolojia ilivyo lazima akila ya haka katoto ikaambie sasa umetoboa kilichobaki ni kumaliza chuo ukaingia kwenye ajira

Hapo bado hajaanza kuwaza eti ooh nikikosa ajira nitaajijiri sababu fursa naziona nyingi kisa tu kawa motivated na motivational speaker .

Ndugu wengi hawasomi ili kuangalia ni kipi anasoma na vipi atapata kazi au kitamsaidia mtaani wao kitu cha kwanza ni kupata boom na la pili awe katika good and known and famous university kamaliza anaamini hapo ndiyo tayari ashatoboa .

Ndiyo maana wakimaliza wanahaha mtaani maana kwanza expectation zinakuwa zinasoma zero ni hapo ndugu kama hawana elimu wanauliza huyu si alikuwa analipwa huko chuo ? Mbona sasa hizo hela hakuzitunza .

Basi hapo lazima dunia iwafunze maana sio wazazi tena .

Nisameheni wadogo zangu sio wote mko hivyo ila asilimia kubwa mko hivi .

Badilikeni mtaani ni kugumu ajira hakuna na pia kujiajiri sio kukaa na kusema nitaajiajiri jiandae kuna mengi ya kujifunza kabla haujajiajiri .

Ikiwa muda unakuruhusu embu kasomee kitu chenye kuweza kukuweka mjini au kwenye ajira kwa asilimia kadha wa kadha

Alafu boom sio hela ya kuwatumia wazazi na kujenga kwenu ni hela ya kujikimu japo ukiweza basi itunze kidogo kidogo ikusaidie pindi umalizapo .

Mnisikie maana wenzenu wako huku wanaalaani kusoma eti walipoteza muda .

Cc mpwayungu village
 
Extra miles ushamaliza kila kitu
No more.
Hakuna aliyekuwa mwamba, tena jiwe kama mimi ila saivi nikipata mteja wa buku namkimbilia hadi jasho linatoka
Pole sana mkuu, ila kwa sasa sheria za uchumi zineshabadilika sana ila bahati mbaya tumeng'ang'ana na sheria za zamani hasa mifumo ya elimu na namna biashara inavyofanyika haitazami mabadiliko ya kiteknolojia.
 
Mimi nafikiri ni asili ya mtazania u much know maana utakuta mtu sio mtaalamu wa kada flani lakini anavyo ya chukulia mambo utabaki unaashangaa sasa ikiwa amepata elimu ya chuo yeye si ndio anakuwa kila kitu mtaani
 
Hao vijana siyo tatizo, tatizo ni mazingira au mfumo unaowaandaa ili waweze kuwa au ku-perform kulingana na matarajio.
 
wabongo wengi tuna ulimbukeni wa mambo, hao madogo wanareflect akili zetu wengi, ipo siku nao watashauri kama unavyoshauri mkuu and the cycle goes on
 
Back
Top Bottom