the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Baadhi ya viongozi wa dini wa Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wamewasihi wanasiasa kuwa na hofu ya Mungu, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ili kudumisha amani ya taifa. Aidha, wameeleza kuwa hawaungi mkono wanasiasa wenye kauli za vitisho na zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Wito huo umetolewa Februari 20, 2025, wakati wa maombi na dua ya kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Maombi ambayo yalifanyika nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Nusrat Hanje.
Mchungaji Joseph Roche, kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship wilayani Ikungi, amesema Watanzania hawapaswi kuishi kwa hofu wakati wa uchaguzi, kwani baada ya uchaguzi maisha lazima yaendelee.
"Hatuungi mkono wanasiasa wenye kauli za vitisho wanaotaka kuvuruga amani na kusababisha hofu kwa Watanzania," amesema Mchungaji Roche.
Kwa upande wake, Kaimu Shekhe wa Wilaya ya Ikungi, Omary Salmu, amesisitiza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuepuka kuwa mashabiki wa uchaguzi, kwani jambo hilo linaweza kuhatarisha amani wakati wa mchakato wa uchaguzi.
Soma Pia: