PreGE2025 Baadhi ya vyama vya upinzani vyasifu Demokrasia kuimarika awamu ya sita

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mwenyekiti wa Chama cha AdaTadea na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib.

WADAU wa siasa wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuimarisha demokrasia.

Mwenyekiti wa Chama cha AdaTadea na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib amesema katika miaka minne ya uongozi wa rais Samia, demokraisa imeimarika.

Khatib alilieleza HabariLEO kabla ya Rais Samia vyama vya siasa vilikuwa vina hali ngumu kutokana na katazo la kufanya mikutano ya hadhara lakini sasa hali ni tofauti.

Alisema pia serikali imeliboresha baraza hilo kwa kulitengea fedha kuliwezesha lifanye shughuli zake.

“Sasa hivi tuna bajeti hivi karibuni Machi 11 hadi 13 Baraza la Vyama vya Siasa na wajumbe wa vyama mbalimbali tulikuwa mkoani Morogoro katika mkutano, sasa hivi tunaweza kufanya vitu vingi tofauti na awali,” alisema.

Ameiomba serikali itoe ruzuku sawa kwa vyama vyote vya siasa ili visivyo na uwezo vifike kwa wananchi kunadi sera zao.

“Inabidi tuzunguke nchi nzima lakini kuna baadhi ya vyama havina uwezo wa kufanya hivyo, mfano mimi nataka kugombea urais Zanzibar na mwenzangu atagombea bara tupewe uwezo wa kuzunguka kote ili uchaguzi ukiisha tusema tumepambana wote lakini wananchi wamekuchagua wewe,” alisema Khatib.

Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Mwanza, Iddi Kiula alisema falsafa ya Rais Samia ya 4R (maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upaya) imepunguza vikwazo katika demokrasia.

Ameiomba Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) isimamie sheria katika uchaguzi mkuu ujao baadaye mwaka huu kwa kuzingatia haki na weledi na iwatangaze watakaoshinda kihalali.

“Rutuba ya demokrasia ni haki, haki itendeke kwa kuhakikisha kuwa tunalolifanya lina maslahi kwa wote kwa kufanya hivyo nchi itaendelea kujengeka,” alisema Kiula.

Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Richard Lyimo alisema demokrasia nchini imeimarika ikilinganishwa na awali.

Alisema Rais Samia amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kurejesha ruhusa ya vyama vya siasa kufanya mikutano.

Lyimo alisema ili kuimarisha demokrasia iliyopo ni muhimu serikali iifanyie kazi hoja ya vyama vya upinzani ya Katiba mpya.

“Baada ya uchaguzi nafikiri ni muda mzuri wa kulifanyia kazi suala hilo, wengi wanalalamika lakini naamini Rais Samia atalifanyia kazi maana ni msikivu,” alisema.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Richard Feruzi alisema falsafa ya 4R imeimarisha demokrasia nchini.

“Baada ya kuingia madarakani kupitia maridhiano tumeona viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ambao walikuwa nje wakirejea nchini mfano Tundu Lissu, Lema na Wenje hii ni ishara ya demokrasia kurudi nchini,” alisema.

Chanzo: Habari Leo
 
dhamira na nia njema ya DR.Samia Suluhu Hassan imejengwa katika misingi ya maneno na matendo.

hayo yote ni matokeo ya falsafa ya 4Rs na mapendekezo ya kikosi kazi, na huo ni mwanzo tu, mengi mazuri zaidi yanakuja :NoGodNo:
 
Pumbavu kabisa hao vibaka, hawajasimamisha hata wagombea kwenye serikali za mitaa ndiyo maana upumbavu uliofanyika 2024 hawajauona shenzi kabisa nguruwe hao.
 
ni Tlaatlaah tu aliye ipenda hiyo article hapo juu. labda ndugu zake watakuja kumuunga mkono muda si punde- this speaks volume.
 
gentleman,
hayupo mtua anependa kuona ukweli kama huo ulioelezwa na huyo mwenyekiti wa ADA TADEA ambae pia ndie mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa Tanzania.

Zamani hawakua hata na posho,
lakini baada ya 4Rs za Dr.Samia Suluhu Hassan na mapendekezo ya kikosi kazi, hata mahudhurio ya vyama vya siasa hususan upinzanzi yamekua bila kukosa kwasababu kuna posho.

Kwahiyo ndugu zangu, friends ladies and gentleman,
Dr. samia suluhu hassan atakumbukwa kwa namna ambavyo ameimarisha demokrasia nchini Tanzania licha ya kwamba hata watu wa no reform no elections zamani walikua hawahudhurii vikao, lakini baada ya posho kuwepo sasa wanahudhuria kikamilifu vikao vya baraza la vyama vya siasa bila kukosa wala kuchelewa:NoGodNo:
 
Back
Top Bottom