Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Tanzania lapendekeza makato ya mishahara kupambana na corona virus

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Tanzania lapendekeza makato ya mishahara kupambana na corona virus

Wanaotakiwa kukatwa mishahara ni wabunge maana ndo wanalipwa mishahara na maposho kibao, sijui milioni kumi na ngapi kwa mwezi. Watumishi wa umma asilimia kubwa mishahara yao haizidi milioni moja, ukiweka makato wanajikuta na laki tatu na hapo hapo hawajaambulia chochote miaka hii mitano, ngoja tusubiri tuone hao wakataji watakata bei gani kwenye hii 150,000/= ya mwalimu hapo juu..
 
Naona Watanzania wengi hatupendi maendeleo, tunataka vitu vidogo vidogo tu. Corona imekuwa kisingizio tu, ila wanasiasa wengi hawataki kuona mafanikio yanakuja Tanzania, tunakuwa kama kuna laana, kwanini waone miradi mikubwa tu na wasione vitu vingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu serikali ikisikiliza huo ujinga na kusitisha hiyo miradi na contractors kutushtaki kwenye mahakama za "ki-miga" hao contractors watashinda. Baada ya hapo ndege (mali) zetu zitaanza kukamatwa huko nje.

Guess what? Wapuuzi haohao watakuja kuilaumu serikali kwa kutuingiza hasara. Tatizo wengi wanaopinga maendeleo akili zao kama za panzi, hazina kumbukumbu.

Rejea suala la ile barabara ya Bagamoyo. Ni bunge lililoishinikiza serikali kuvunja mkataba na mkandarasi baada ya kupuyanga. Alipokuja kupewa tuzo mahakamani huko Ufaransa na ndege yetu kukamatwa Canada, tarumbeta zikaibuka kuisiliba serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye majina ya hao wabunge aweke tuwajue ila naamini hawawezi kuwa "wale jamaa".
 
Bajeti ya mwenge inatosha,waachane na mishahara,wagonjwa wenye 20!
 
Chadema kama chama kikuu cha upinzani wanapaswa kuonyesha njia mbadala au kuwa mfano kwa kufanya mambo " mema" ambayo CCM hawakuyatilia maanani.

Mfano pale Kenya baadhi ya wabunge wameomba kukatwa kati ya asilimia 30 hadi 50 ya mishahara yao kusaidia mapambano haya nchini mwao. Huko Ulaya kama UK, France na Spain wabunge wamechanga na kusababisha watu wa kada nyingine kuiga mfano.

Hapa Tanzania nimewaona wafanyabiashara wakichangia mfano Rostam Aziz na wengine wengi.

Chadema mnaweza kutuongoza watanzania katika kuchangia janga hili la Corona kwa sababu mna uzoefu na mambo haya ya michango.

Nawatakia Pasaka yenye baraka.

Haleluya....... Haleluya........Haleluya!

Maendeleo hayana vyama.
 
We said from day one kuwa mamiradi yanayokausha fedha yasitishwe haraka. Tangu Januari tungekuwa na Trillion zaidi ya 10. Tungeweza kukabiliana na tatizo lolote la kiuchumi.

Magufuli akajifanya mjuaji akaagiza hakuna kitu kitakachosimama. Sasa makampuni yamefunga kila kitu, TRA wameshashindwa kukusanya fedha hata nusu ya miezi iliyopita. Sijui hawa watu wanawaza nini mpaka sasa.

Ila yawezekana Mungu amewafumba macho wasione yanayokuja siku za usoni.
Juzi nilipoona waziri wa nishati akikomaa eti ujenzi wa bwawa jipya haujawahi kusimama na hautasimama kamwe nikasema hatuna viongozi tuna "Kiki Mongers"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom