Tetesi: Baadhi ya wabunge wa viti maalum CHADEMA, kupokelewa CHADEMA makao makuu Juni baada ya bunge kuvunjwa

Tetesi: Baadhi ya wabunge wa viti maalum CHADEMA, kupokelewa CHADEMA makao makuu Juni baada ya bunge kuvunjwa

Hata mimi Hawa wabunge wakirudi Chadema nitaumia sana. Hawatakiwi kukaa na watu wanafiki na wazandiki kama Chadema.
sasa maumivu makali utakayopata si uyatafutie ufumbuzi binafsi kama ilivyo kwa wenye chuki binafsi wengine gentleman 🐒
 
Huenda hatma ya uanachama wa wabunge wa viti maalumu wa chadema, maarufu kama wabunge wa COVID-19, ikajulikana mara tu ya bunge kuvunjwa. Inasemekana watapokelewa kwa mapokezi maalumu rasmi chadema mwezi June mwaka huu, mara baada ya ya vikao rasmi vya maridhiano na muafaka wa pamoja kufikiwa.

Wabunge hao waliotengwa na chadema tangu mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, wataendelea na shughuli zao mjengoni huku mazungumzo yasiyo rasmi baina yao na uongozi mpya wa Chadema taifa yakiendelea vizuri na kutoa matumaini ya muafaka mwema wa pamoja kufikiwa baina yao, huenda ikawa mapema zaidi hata kabla ya mwezi June, muda wa mwisho uliowekwa kuelekea uchaguzi mkuu. Haya yote yanatokea na kufanyika, baada ya mvurugano wa kisheria ngazi ya chama na mahakamani kwa takribani miaka mitano iliyopita.

Taarifa za chini ya kapeti kadiri alivyodokeza mnyetishaji wa tetesi hiii, zinaeleza kwamba wabunge hao tayari wamezilipia kadi zao za uanachama kwa muda mrefu zaidi, lakini pia wanauunga mkono uongozi mpya pamoja na uelekeo wake, na tayari wameupokea vizuri sana hata wito wa mwenyekiti wa Chadema taifa, kwa wanachama na wadau wa chama hicho kukichangia chama hicho kwa hali na mali ili hatimae kipate nguvu ya rasilimali fedha kujiendesha. Na tayari baadhi yao wameshachangia kwa njia ya mtandao na kiasi kingine kimewasilishwa HQ kama ujumbe maalumu kwa uongozi mpya.

Mazungumzo rasmi baina ya wabunge hao na uongozi mpya wa Chadema yanasemekana yanaweza kuanza wakati wowote kuanzia sasa, ili hatimae kua na muafaka wa pamoja mapema iwezekanavyo kwasababu wabunge hao wanahitajika zaidi ndani ya chadema, kuliko wao wanavyohitaji kurudi chadema, kutokana na nguvu ya ushawishi walionao kwenye chama na jamii kwa ujumla.

Ifahamike kwamba sio wabunge wote watakaorejea chadema, baadhi yao wanaelekea vyama vingine vya siasa na kuendelea na maisha mengine.

Ndugu mdau una maoni gani na uelekeo huu wa Chadema na wabunge hawa wa viti maalumu?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Mnakaribishwa wote enyi wabunge wa viti Maalumu.

Ila wewe Mchepuko wa Mbowe UBUNGE basi tena
 
Majuto ni mjukuu. Hawa Wabunge sasa hivi wanajuta sana kwa kitendo chao cha kujipeleka Bungeni. Wangevumilia miaka hii mitano hakika wangerudi mjengoni. Bunge lijalo CHADEMA watakuwa na Wabunge wengi mjengoni. Sidhani kama wanaweza kurudishwa hivi hivi bila kutoa sababu ya kuingia Bungeni bila baraka ya Chama.
kurudi mjengoni sifahamu,
ila watapokelewa chadema HQ kwa kishindo kikuu mwezi June na kiongozi mpya wa Chadema 🐒
 
relax gentleman,
huna haja ya kupanic kwa mihemko, just be informed kwamba pesa ni kitu mzuri sana, hata uwe mkali mwenye mdomo na makelele kiasi gani pesa na asali ikiwekwa mdomo pako unatulia tu kama kibaka na tapeli wa siasa ndani ya chadema alivyotulizwa 🐒
Tulia we 🌈
 
Back
Top Bottom