Tetesi: Baadhi ya Wachezaji wa Tabora United watelekezwa, wanatafuta nyumba za kupanga kwa gharama zao

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936


HILI LA TABORA NI KIBOKOšŸ™Œ

Baadhi ya wachezaji wa Tabora United wameonekana mitaani wakiwa na watu wanaodaiwa kuwa madalali, wakiwatafutia nyumba za kupanga baada ya uongozi wa timu hiyo kuwatelekeza katika nyumba ya wageni walikokuwa wakiishi tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu huu.

Chanzo changu kimenifahamisha kuwa baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Fountain Gate, mmoja wa viongozi wa timu aliwapa taarifa wachezaji 16 wazawa kuwa muda wa kukaa katika nyumba ile ya wageni umeisha, na waliagizwa kuondoka kesho yake saa nne asubuhi na kutafuta vyumba vya kupanga mitaani kwa gharama zao, kwa kuwa wanalipwa mishahara.

Hata hivyo, wachezaji hao walijichangisha na kupanga nyumba moja kwa muda mfupi huku wakitafuta vyumba vingine. Mpaka Jumapili usiku, baadhi yao bado walikuwa hawajapata nyumba za kupanga, na hivyo kulazimika kujiweka katika nyumba za wageni (guest houses) kwa gharama zao.

Chanzo changu kimeeleza kuwa baadhi ya wachezaji (majina yanahifadhiwa) wamegoma kwenda mazoezini kwa sababu hawaelewi kinachoendelea, na uongozi haujui wanakula chakula gani na lini. Wanachotaka ni kufika mazoezini lakini hali yao ya maisha imekuwa ngumu.

NB: Wachezaji 12 wa kigeni hawahusiki na matatizo haya, kwani wao wanaishi kwenye apartments za kifahari maeneo ya Uzunguni kwa gharama za timu.
 
Mikataba inasemaje? Watapewa na makazi ama? Kama mikataba inasema watapewa makazi wadai, kama haisemi hivyo, basi kila mmoja nyumba yake ni mfuko wake.
 
JAPANESE UNCENSORED
 
Alafu tff ilimpatia kolo aanze Naye.
 
Kama we ni mchezaji na unapata mazingira kama hayo kwanini wakihongwa wakatae kupanga matokeo,wachezaji kukaa nyumba moja inarahisisha kufikiwa hata na makampuni ya kubet kupanga matokeo kama inavyotekea kwenye vitimu vya Kenya.
 
Kwani wangesajili wachezaji watano wa kigeni, halafu wanaobaki wakawa wazawa na kuwapa maslahi mazuri kulikuwa na ubaya gani!
 
Sasa si wanalipwa mishahara si wakapange
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…