KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
HILI LA TABORA NI KIBOKOš
Baadhi ya wachezaji wa Tabora United wameonekana mitaani wakiwa na watu wanaodaiwa kuwa madalali, wakiwatafutia nyumba za kupanga baada ya uongozi wa timu hiyo kuwatelekeza katika nyumba ya wageni walikokuwa wakiishi tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu huu.
Chanzo changu kimenifahamisha kuwa baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Fountain Gate, mmoja wa viongozi wa timu aliwapa taarifa wachezaji 16 wazawa kuwa muda wa kukaa katika nyumba ile ya wageni umeisha, na waliagizwa kuondoka kesho yake saa nne asubuhi na kutafuta vyumba vya kupanga mitaani kwa gharama zao, kwa kuwa wanalipwa mishahara.
Hata hivyo, wachezaji hao walijichangisha na kupanga nyumba moja kwa muda mfupi huku wakitafuta vyumba vingine. Mpaka Jumapili usiku, baadhi yao bado walikuwa hawajapata nyumba za kupanga, na hivyo kulazimika kujiweka katika nyumba za wageni (guest houses) kwa gharama zao.
Chanzo changu kimeeleza kuwa baadhi ya wachezaji (majina yanahifadhiwa) wamegoma kwenda mazoezini kwa sababu hawaelewi kinachoendelea, na uongozi haujui wanakula chakula gani na lini. Wanachotaka ni kufika mazoezini lakini hali yao ya maisha imekuwa ngumu.
NB: Wachezaji 12 wa kigeni hawahusiki na matatizo haya, kwani wao wanaishi kwenye apartments za kifahari maeneo ya Uzunguni kwa gharama za timu.