Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Baada ya kuripotiwa kuwepo kwa mgomo kwa wafanyabiashara Mkoani Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, pia leo June 26, 2024 baadhi ya wafanyabiashara Mkoani Iringa nao wamefunga maduka yao.
Mmoja kati ya wafanyabiashara ambaye naye amefunga duka lake, amesema kuwa nao wamechukua uamuzi huo kwa sababu baadhi ya madai yanayolalamikiwa na wafanyabiashara wa Kariakoo yanawagusa na wao.
Ikumbukwe mgomo huo ulianzia Jijini Dar es Salaam kwenye Mkoa wa kikodi wa Kariakoo june 24, 2024 ambapo baadhi ya maduka yameendelea kufungwa licha ya kuwepo kwa taarifa ya kufanyika kikao cha majadiliano baina ya wawakilishi wa wafanyabiashara na Serikali.
Ambapo katika kikao hicho ilielezwa Serikali kuchukua hatua mbalimbali kwenye baadhi ya madai ikiwemo kusitishwa kwa zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu rafiki wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.