Baadhi ya wageni huwa sio wastaarabu kabisa

Baadhi ya wageni huwa sio wastaarabu kabisa

Nyamwage

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
712
Reaction score
1,748
Hi,

Tabia zako zinatosha kukuelezea wewe ni mtu wa aina gani. Imagine mgeni anafukuafukua msosi kama yuko mgodini kutafuta nyama, lengo lake ni nini au anataka wenyeji tule pilau kavu?

Binadamu wengine jau kweli, hawa ndio wale ndugu akifa wanakuja kung'ang'ania mali ambazo hawajui hata zilipatikana vipi!
 
Wengine ni kero zaidi hasa kwenye suala kula. Kwa milo yenye matunda unakuta mgeni anajaza sahani mlima mkubwa bila kujali kuna wenzake nao watajipakulia, matunda anakula tunda zima badala ya kipande kimoja.

Yaani ndizi moja watu wawili, chungwa moja watu wawili, mjini huwezi ukala tunda zima wakajti wa mlo utaonekana kituko.

Kama una hamu na matunda nenda kale yale yanayouzwa mitaani ule tani yako. Tena siku hizi wanauza matunda mseto sahani imejaa kwa buku tu.

Wageni wengine wanafunua friji na kujilia watakachokikuta humo. Unarudi kazini jioni unakuta mboga na matunda yameliwa yote kabla ya muda wa milo
 
Mwingine chai anataka anywe kwenye jagi badala ya kikombe, ukimpeleka kula hotelini au mgahawani haoni aibu kuagiza chakula na bei ya juu bila kujali mfukoni mwa mwenyeji wake kuna fedha kiasi gani. Ukienda nae kwenye mualiko anatia aibu kwa kujaza sahani vyakula vyote vilivyopo kwenye foleni ya bufee. Kwenye bufee haitakiwi ufike mpaka mwisho wa foleni ya vyakula, unatakiwa kuruka vyakula ambavyo huwa una vila mara kwa mara, unachagua ambavyo hukutani navyo mara nyingi na usijaze sahani mpaka juu ili kuepuka watu kukushangaa na kukuona ni limbukeni wa vyakula na huna jeuri ya kuvipata
 
Watz tatizo letu hatuna uhakika wa Kesho that way tunachukia Hadi wageni kiss chakula Tena chakula Cha kawaida Kama wali na nyama ambayo kilo moja haizidi elf 8

Njaa tunabidi kuifukuza pika chakula Cha kutosha watu wale washibe
 
Back
Top Bottom