OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Naendelea kufuatilia ahadi mbalimbali za wagombea urais nchini kuelekea Uchaguzi mkuu wa Okt 2025 naona kuna shida nyingi sana kwa wagombea. Wengi hawajui mahitaji ya watanzania ni nini, maana yake wanaleta ndoto ambazo hazina kazi kwa watanzania.
Mathalani, mtu analeta ahadi ya kuzalisha nuclear, unawaza kwani Tanzania ina shida gani hadi iwaze kuzalisha nuklia wakati watu wanaogelea dimbwi la umasikini. Ahadi za vijana kupewa simu, laptop nk ni ahadi ambazo unaona kabisa wagombea urais ni watu wa futuhi/comedy.
Kuna mgombea anazungumzia Ubwabwa, huyu nilimuelewa mwaka 2020 ila alipoenda kuhojiwa nikaona ni mchekeshaji. Maana suala la ubwabwa angeweza kulitafsiri kama Food Security na kuleta maana, baada ya kukomaa na ubwabwa kwa maana ya ubwabwa tu. Suala la Ubwabwa limejitokeza tena kwa kampeni hizi. Hata hivyo ni suala lile lile tu halijakaa kwenye food security na kupunguza idadi ya malnutriouts chiildren au people.
Kwa haya na mengine mengi naona kabisa siasa za Tanzania zinawachekeshaji wengi sana kuliko watu wenye ufahamu na masuala mbalimbali ya nchi ili kulenga mabadiliko. Na hapa sio kama nasema kuna chama kina hoja au sera nzuri, wote ni wazururaji tu, sera bila mkakati na mpango ni uongo uliopitiliza. Mathalani wale wanaoahidi matrekta, kupunguza mikopo nk, hawana mkakati wa kusema miaka kadhaa iliyopita walishindwaje hadi tuamini kuwa miaka kadhaa ijayo watawezaje.
Nawasilisha.