Jambo lingine ni kuwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wamelalamikia kuchangishwa fedha za mafuta katika magari ya kubeba wagonjwa kutoka hospitali hiyo kwenda kupata matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Wananchi wamesema hiyo inakuwa changamoto hususani kwa Wananchi masikini ambao wanaitegemea Serikali kunusuru uhai wao.
Wananchi hao wamesema licha ya Serikali kuwekeza vifaa vya kisasa bado kumekuwepo na huduma mbovu na kuomba Serikali hususani Wizara ya Afya kufika hospitali hapo kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo.
============
Updates...
Kaimu Afisa Uhusano wa Umma wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro, Scholastica Ndunga anafafanua “Ni kweli wagonjwa wanaotumia gari wanachangia hela ya mafuta na hachangii mtu mmoja, kama wapo wawili au watatu wanashirikiana, kwa ambao hawana uwezo wa kuchangia kuna utaratibu wao kupitia huduma za Ustawi wa Jamii.
“Utaratibu wa kuchangia usafiri huo una muda, sikumbuki ulianza lini, kwa kuwa hata unapomhudumia mtu kwa kumpa msamaha lazima useme kwa maandishi, zamani hatukuwa na vitu kama hivyo.”