ThnkingAloud
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 611
- 621
Wakati wa utawala wa JPM aliwahi kuwashukia baadhi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kwa kusababisha serikali kukosa mapato yake halali yatokanayo na kodi.
Aliwaambia ana kwa ana kuwa wanahusika katika kutoa mahesabu yaliyokaguliwa ya aina mbili. Seti ya kwanza ya mahesabu yaliyokaguliwa ni ile inayoonyesha kuna faida ndogo ya kutozwa kodi (au hasara kabisa) ni kwa ajili ya TRA. Seti ya pili ni ile inayopelekwa benki kwa ajili ya kuomba na kupata mikopo ya kibiashara ambayo inaonyesha kampuni imepata faida kubwa kwa mwaka ule ule wa kihasibu na mapato.
Mchezo huu umejirudia baada ya mwenda zake JPM.
Naiomba serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania kupitia Directorate of Bank Supervision ihakikishe jambo hili linakomeshwa kwa kuweka utaratibu wa ukaguzi utakaolikomesha. Au mifumo ya TRA na watoa mikopo wote isomane kuhakikisha mahesabu ya mwaka husika ni yale yale TRA na kwenye mabenki ya biashara.
Iwachukulie hatua kali za kisheria wakaguzi wa mahesabu ikiwa ni pamoja na kuwafutia usajiri wanosaidia kuikosesha serikali mapato kwa njia hii haramu.
Nawasilisha.