Uchaguzi 2020 Baadhi ya wana CCM wanaotafuta nafasi za Ubunge, wameanza usumbufu wa rushwa

Uchaguzi 2020 Baadhi ya wana CCM wanaotafuta nafasi za Ubunge, wameanza usumbufu wa rushwa

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Baadhi ya wana CCM wanaotafuta nafasi za Ubunge, wameanza usumbufu. Mimi siyo mwana CCM lakini leo napigiwa na mtu anayejitambulisha ni Mkurugenzi wa Halmashauri na anataka kugombea na anaomba support yangu.

Namuuliza simu yangu kapata wapi? Anaomba niwe mpole tu tuelewane. Nauliza mbona mapema anasema wako wengi kila mtu anatafuta waungaji mkono.

Finally, ameahidi kunirushia elfu 40! Nazisubiri ili niongeze bando la kuchat JF maana naona hawa CCM rushwa ni sehemu ya vinasaba vya miili yao. Yaani unahongwa hata kabla mtu hajachukuwa fomu!
 
Baadhi ya wana CCM wanaotafuta nafasi za Ubunge, wameanza usumbufu. Mimi siyo mwana CCM lakini leo napigiwa na mtu anayejitambulisha ni Mkurugenzi wa Halmashauri na anataka kugombea na anaomba support yangu.

Namuuliza simu yangu kapata wapi? Anaomba niwe mpole tu tuelewane. Nauliza mbona mapema anasema wako wengi kila mtu anatafuta waungaji mkono.

Finaly ameahidi kunirushia elfu 40! Nazisubiri ili niongeze bando la kuchat JF maana naona hawa CCM rushwa ni sehemu ya vinasaba vya miili yao. Yaani unahongwa hata kabla mtu hajachukuwa fomu!
Huyo ni kama Lissu! Amechukua form tu na hajaijaza mara ana omba kuchangiwa - Afadhali huyo wa CCM anataka aliwe hela yake. Lissu anataka ale hela zako.
 
Hivi hawa kweli sijui wakoje! Kwa utaratibu wao nilihisi sasa hivi wangetulia wasubilie mchujo, lakini eti wanagawa pesa kuungwa mkono! Mkosi nilionao huyu atakuwa amegundua ni namba ya makosa. Ila inanipa picha kwamba watu wa aina hii ubora ni mdogo sana!
 
Rushwa ni sehemu ya wanasiasa wote/walio wengi. Mnaotupa mawe kwa wanaccm mnakuwa biased bila sababu, au ndio kusifu kwa makofi, wanasiasa sio watu safi hata kidogo, wengi maisha yao ni ya ndumba, kumwaga damu na rushwa. Sasa endeleeni kuwa biased na uccm vs uchadema.
 
Huyo ni kama Lissu! Amechukua form tu na hajaijaza mara ana omba kuchangiwa - Afadhali huyo wa CCM anataka aliwe hela yake. Lissu anataka ale hela zako.
Nadhani tuna matatizo ya ubora wa wanasiasa tulionao. Unawezaje kuomba michango hata kabla ya kupitishwa? Kama hii hadithi ya zygot ni sahihi, iweje mtu hata hajachukuwa fomu anaanza kutafuta kuungwa mkono kwa rushwa? Siasa imekuwa ni kazi ya kufa-na-kupona! Ni kwa wajinga na welevu na nadhani majority ni wajinga tu!
 
Mchakato wa kuwapata wabunge this time ni mgumu sana na siyo rahisi kutumia rushwa kabisa, hii ni CCM mpya. Ebu pitia mchakato wa uchaguzi wa majimbo [emoji1313] chini then unambie rushwa itaanzia wapi hapa?

CCM-MCHAKATO WA UCHAGUZI MAJIMBONI 2020

HATUA YA KWANZA

-Kuchukua fomu (Kimyakimya bila mbwembwe)
-Kujaza Fomu
-Kurudisha fomu
-Kujadiliwa na kamati ya siasa wilaya (Wanatoa maoni kwa kila Mgombea, kama wagombea wako 10 au 3 au 7 wote wanatolewa maoni)
-Maoni hayo kwa Majina ya wote waliochukua fomu yanapelekwa Kamati ya siasa Mkoa kujadiliwa.

HATUA YA PILI
-Kamati ya siasa Mkoa inajadili majina ya watia nia wote toka Wilayani/Majimbo.
-Kamati ya siasa Mkoa inatoa maoni kwa kila mtia nia.
-Kamati ya siasa Mkoa inapeleka Majina Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

HATUA YA TATU

-Halmashauri Kuu/Kamati Kuu kujadili majina ya watia nia toka wilayani.
-Halmashauri Kuu/Kamati kuu kuchuja majina ya wagombea(Kama walikuwa 3,10 au 7) wanachuja na kubaki majina 3.
-Majina matatu yanafungwa kwenye bahasha ya SIRI na kurudishwa wilayani/Jimboni.
-Kwenye Mkutano Mkuu wa wilaya/Jimbo ambao huwa unakuwa na wajumbe kati ya 800 hadi 900.Majina matatu yatasomwa hapo.
-Kumbuka wakati Majina yanasomwa, watia nia wote wanapaswa kuwepo ili wasikilize kama wameteuliwa au wamekatwa.
-Mkutano Mkuu wa Wilaya utapiga kura kwa Majina hayo 3 yaliyosomwa, kisha matokeo yanatangazwa(Mchakato hauuishi hapo)

HATUA YA NNE
-Matokeo ya majina matatu kama yalivyopigiwa kura yanapelekwa KAMATI KUU ya CCM TAIFA.
-KAMATI Kuu ya CCM Taifa itatangaza jina moja kati ya yale matatu.

-Jina hilo linapelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwaajili ya taratibu za Uchaguzi Mkuu.

CCM MPYA 2020
 
Kamati kuu kwa maelezo hayo imepewa nguvu kama za yule wa kule ....
 
Hivi kuna MTU anaweza kuitenga CCM na Rushwa? Kwa mfano, hii ya kuprint form moja pekee, haiwezekani ikatafsiriwa kama Rushwa kama ni kweli??

CCM ndio yao Rushwa
Pammoja na kulamba bingo ya elfu 40,lakini majina matatu ndio mtayapigia kura,sasa anajuaje kama hatakatwa juu kwa juu?Au ameisha toa bahasha nzito ngazi ya taifa?
 
Hivi kuna MTU anaweza kuitenga CCM na Rushwa? Kwa mfano, hii ya kuprint form moja pekee, haiwezekani ikatafsiriwa kama Rushwa kama ni kweli??

CCM ndio yao Rushwa
Na hilo la kuprint fomu moja ni kama kuwatangazia wana CCM wote kuwa miongoni mwao hakuna mwenye uwezo wa kufanya zaidi ya aliyepo madarakani
 
Back
Top Bottom