Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Hichi ndicho kinachoendelea vichwani mwa baadhi ya wanaCCM baada ya Polepole kulipua kambi ya kijani siku ya jumapili na kisha leo kuibuka upya na petrol kuteketeza kambi nzima ya kijani.
Makada wa kijani wameshindwa pakuanzia maana mama mkuu hajatoa muelekeo wa namna ya kujibu mapigo. Huenda labda hofu imemtanda au anasoma upepo.
Kilichofanywa na Polepole kinatafsiriwa kama ni upasuaji mkubwa uliofanywa na Daktari bingwa wa kupasua, lakini akaamua kupasua bila mgonjwa kupigwa dawa za nusu kaputi na kushonwa hivyo hivyo bila ganzi. Lakini kabla mgonjwa hajapata nafuu kubwa, Daktari yule yule akarejea upyaa kufumua mshono bila mgonjwa kupigwa nusu kaputi, na safari hii kidonda hakijashonwa kabisa, kiko wazi.
Ni mwendo wa CCM kupigwa operesheni kubwa kubwa bila ganzi.