DOKEZO Baadhi ya Wanafunzi Darasa la 7 Shule ya Msingi Mitundu B, Singida wanasoma hadi usiku bila kula

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mitundu B, Singida wanabaki shuleni hadi usiku kwa ajili ya masomo ya ziada (prepo), licha ya baadhi yao kutokuwa wamekula tangu asubuhi.

Waliambiwa wachangie chakula ili wakae kambini na kusoma usiku, hata hivyo, baadhi ya wazazi hawakuweza kuchangia kutokana na kukosa uwezo wa kifedha. Badala ya wanafunzi hao kuruhusiwa kwenda nyumbani kupata chakula, wanalazimishwa kuendelea na masomo bila kula.

Hali hii inatia wasiwasi kwa sababu mwanafunzi anayesoma akiwa na njaa anaweza kushindwa kuelewa masomo na pia kuhatarisha afya yake.

Tunaomba Uongozi wa Shule, Halmashauri na mamlaka za elimu kufuatilia suala hili na kuhakikisha hakuna mtoto anayelazimishwa kusoma usiku bila kupata chakula au kuwekwa katika mazingira yanayoweza kuhatarisha usalama na ustawi wake.

Pia soma ~ Itigi DC: Wazazi watatu ndiyo hawajatoa michango ya chakula Shule ya Msingi Mitundu B ila Watoto wao wanapewa chakula
 
Hii mbaya sana watakuja kuua watoto! Unakuta mtoto anapimwa sukari 24 damu 5

Huu ni uuaji wa kuishinda bila kula na kusoma bila kupumzika
 
Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mitundu B, Singida wanabaki shuleni hadi usiku kwa ajili ya masomo ya ziada (prepo), licha ya baadhi yao kutokuwa wamekula tangu asubuhi.

Waliambiwa wachangie chakula ili wakae kambini na kusoma usiku, hata hivyo, baadhi ya wazazi hawakuweza kuchangia kutokana na kukosa uwezo wa kifedha. Badala ya wanafunzi hao kuruhusiwa kwenda nyumbani kupata chakula, wanalazimishwa kuendelea na masomo bila kula.

Hali hii inatia wasiwasi kwa sababu mwanafunzi anayesoma akiwa na njaa anaweza kushindwa kuelewa masomo na pia kuhatarisha afya yake.

Tunaomba Uongozi wa Shule, Halmashauri na mamlaka za elimu kufuatilia suala hili na kuhakikisha hakuna mtoto anayelazimishwa kusoma usiku bila kupata chakula au kuwekwa katika mazingira yanayoweza kuhatarisha usalama na ustawi wake.
Primary prepo ya nn sasa mpaka usiku mwishoni unasikia kuna mtoto kabakwa anasingiziwa boda boda
 
Back
Top Bottom