McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Hali ya sintofahamu imejitokeza katika eneo la Bon City, mtaa wa Mlimani, kata ya Murieti, jijini Arusha, baada ya wananchi kulalamikia machinjio yanayodaiwa kuhatarisha afya na mazingira ya wakazi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa wananchi, machinjio hayo hutumika kuchinja kondoo wanaodaiwa kutolewa kama sadaka na mtu mwenye asili ya Kiarabu. Hata hivyo, wamedai uchinjaji huo hufanyika katika mazingira yasiyo salama na yasiyokidhi viwango vya usafi, hali inayozua hofu ya athari za kiafya kwa wakazi wanaoishi jirani.
Uchunguzi wa Kusaga TV umebaini kuwa licha ya machinjio hayo kudaiwa kufungwa mara kadhaa na mamlaka husika, shughuli zake zimekuwa zikiendelea tena, jambo lililozua maswali kuhusu utekelezaji wa sheria na usimamizi wa mamlaka zinazohusika.
Baadhi ya wananchi wamesema hawapingi utoaji wa sadaka kwa watu wenye uhitaji, lakini wanasisitiza kuwa misaada hiyo inapaswa kutolewa kwa kuzingatia sheria, usafi na usalama wa mazingira. Wamedai kuwa umaskini wa baadhi ya wananchi haupaswi kutumiwa kama sababu ya kupuuza taratibu zinazolinda afya ya jamii.
Baadhi