Baadhi ya wananchi Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya wametishia kutokushiriki uchaguzi Mkuu Oct ,2025 wakidai kuwa mgombea aliyeshinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo sio chaguo la wananchi ni chaguo la chama.
Wananchi wa jimbo hilo wametuma ombi kwa uongozi wa chama cha mapinduzi Taifa ,kurejesha jina la mgombea ambae ni chaguo la wananchi na wanaimani nae kuwa atawaletea maendeleo.
Na baadhi ya wajumbe ambao ndio wapiga kura wameomba Chama chao kiruhusu mchakato wa kupiga kura urudiwe ili uwe huru na haki.