Asili ya mwanamke ni pambo za tabia njema,uadilifu na uaminifu toka enzi na enzi ,mwanamke akibeba zege watasema kama dume vile ila mwanaume akipika hawasemi kama mwanamke vile
Wanawake baadhi wa sasa hivi kwa kweli sijui ni wa sayari gani,kwa sababu tuna hulka mbaya mbaya ambazo ukiambiwa unajiuliza hivi huyu ni mwanamke ametoka kwenye mifupa ya wazazi au kashushwa?
Sio wote lakini wengi sasa hivi wana tabia mbaya jamani,tumekua tukishuhudia majambazi ya kike mpk unashangaa,achana na ujambazi utapeli siku hizi wadada hawana mpinzani(sio wa kimapenzi)yaani wanatapeli Mali mchana kweupe,kuna wezi hao ndo usiseme wizi mdogo mdogo na mkubwa yaani zile tabia za ajabu za kiume sasa hivi sisi ndo tumebeba,kuna video mbali mbali zinarushwa wanawake wamekamatwa waanaiba maduka ,nguo,cheni n.k mmoja niliona kakamatwa anaiba kanisani[emoji3][emoji16][emoji16]
Hivi tumekosa utashi kiasi hicho wamama...ifike mahali turidhike na hali zetu hakuna maisha magumu kama ya kuigiza au ya kwenye video unataka ufanane na Fulani badala ya kujikubali
Siku moja tulienda kwenye kitchen party na mwenzangu sasa tumepiga picha mda wa kugomboa nkalipia nafika mbel ananionyesha picha nyingine ya kwetu eti aliiba kwa kua hatuigomboa...nilichoka sana!!
Huko kwenye sosho media kuna wanaoijfanya wanauza vitu online hao ndo matapeli vibaya anakuambia tuma hela,ukituma umeliwa hapatikani...yaani sasa hv wanawake zile tabia ambazo tulikua tunawasema wanaume naona na sisi ndo tunazivaa...najua humu hamna wenye hizo ila wasomaji wapo wengi...
Tubadilike kwa kweli tuwe na hofu ya Mungu sisi ndo walezi na sisi ndo kiigizo cha watoto wetu!!!