Kama ulikusudia "upofu" kumaanisha kushindwa kung'amua naona wewe ndiye una "upofu" mkubwa wa aina hiyo kuliko hao unaowasema.
Kwanza ni offensive (and yes sooo 20th century) kuhusisha conditions za watu na mapungufu ya ung'amuzi au mengine yeyote yasiyotokea naturally.It is not cool to say "Muogope kama Mkoma" anymore.It is germophobic. Will Smith katika wimbo wake "Live at Union Square" (1986) alisema
I want everybody out there that's ugly
all the ugly people be quiet
all the filthy, stinky, nasty people be quiet
all the homeboys that got aids be quiet
all the girls out there that don't like guys, be quiet
hold on, wait a minute
all the girls that don't like guys be quiet
Leo hii anajisikia very embarassed kwa sababu ni maneno yanayoonyesha ujinga wake kuhusu matatizo haya.Anaweza kusamehewa kwa sababu ilikuwa 1986, alikuwa mdogo sana na hata haya mambo nayo yalikuwa relatively mapya
Ni basi tu hatupo katika society iliyo au inayotaka kuwa completely politically correct.Otherwise wengine tungekuwa justified kuona kuhusishwa kwa wale walio "visually challenged" na kutojua mambo ni kashfa.Kuna mtu wa aina hii ni Gavana wa jimbo la New York, sasa unaposema Watanzania ni vipofu maana yako nini?
Kuna kina Nico Zengekala, Kina Mzee Morris Nyunyusa na kuna mpiga ngoma mwingine maarufu kipofu jina nimemsahau, sasa hawa achievement zao ndogo? Kuna watu wana vision zao na hawawezi kuimba au kupiga ngoma kama hawa.
Kwa hiyo tukitaka kusema Watanzania hawajui kitu tusitumie mifano offensive na ambayo inawabagua watu fulani wa society.Sema Watanzania wamezubaa, wajinga, hawana akili etc usiseme Watanzania vipofu. Vipi vipofu wanaoelewa mambo na ambao hawapigii kura wala kushabikia uzandiki huu unaoukashifu, wao watakuwa vipofu wa aina gani? watakuwa vipofu wa aina zote mbili metaphorically and literary au watakuwa "vipofu wanaoona"?
Hilo la kwanza na wengine wanaweza kuliona trivial, lakini liko deep in our collective subconscious as a nation.Ukiwa na attitude kuwa vipofu ni watu wasiojua hukawii kuwa condescende na hata kuwa abuse.Kuna vipofu wanaojua kusoma (braille) na wengi wenye macho wasiojua kusoma!
Lakini zaidi ya hapo, tukiondoa swala la matumizi mabaya ya lugha na mifano, kuna swala zima la kutoelewa nature ya Watanzania.Watanzania wana complexity inayo defy conventions nyingi tu.Trust me, hawa watu wanaelewa due process kuliko tunavyofikiri na inawezekana wengi wana suspend judgement, of course kuna ma partisan ambao kila mtu wa CCM hakosei, of course kuna ma opportunist wanaojua Chenge ana vijisenti kwa hiyo tusicheze mabali, of course kuna ma radical kama yule mchizi wangu aliyemkata Kikwete mtama kwenye campaigns, kwa hiyo kuna kila mtu wa kila hali tanzania.Usione hao wachache waliojitokea barabarani kuangalia commotion ya magari pamoja na kuamini ripoti za magazeti uchwara yaliyonunuliwa ukafikiri Chenge ana mass appeal na support kiasi hicho.Ikumbukwe Bariadi ni moja ya sehemu zenye upinzani mkubwa kwa CCM na hata kama DP inachechemea bado networks zake huko kwa kina Cheyo zipo.
Sitaki kudismiss argument yako kuwa kuna watu hawajui kinachoendelea, na mara nyingi tumejadili jinsi ya kupanga mikakati ya kuongeza elimu ya uraia nchini.Lakini pia kuna hii elitist attitude ya kuwa "sisi ndio tunajua kinachoendelea, watu wa vijijini hawajui kitu" inakosa adabu na haijui kuwa ushamba wa ushamba nao ni ushamba! Kwamba kama vile baadhi ya watu wa vijijini walivyokosa elimu ya magharibi na wasivyosoma magazeti, na sisi inawezekana tumekosa elimu ya asili na hatujui ku reason kivyao.Kuna mababu/ mabibi wengi wana akili na busara sana bila shule.Tunafanya juhudi gani kuungana nao, kuwasikiliza na kuwaelewa kwa nini wanapigia kura CCM?
Tukiweza kujibu hili swali, bila ya kufanya assumptions za haraka haraka za elimu -ya magharibi- ndogo (inaweza kuwa factor but lets find out) tutakuwa na sehemu nzuri ya kuanzia.