SI KWELI PreGE2025 Baadhi ya watia nia wa CCM tayari wamepitishwa na kamati kuu kugombea kwenye majimbo yao

SI KWELI PreGE2025 Baadhi ya watia nia wa CCM tayari wamepitishwa na kamati kuu kugombea kwenye majimbo yao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
CCM21JULAI2025.jpg
 
Tunachokijua
Julai 15, 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitoa taarifa kwa umma kikieleza kuhusu kikao cha kawaida cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichotarajiwa kufanyika tarehe 19/7/2025 saa 4:00 asubuhi jijini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo sehemu ya agenda ilikuwa ni kupokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wa Jimbo na Viti Maalum.

Baadaye Julai 19, ilitolewa taarifa kusogeza mbele Vikao vya Chama hicho ambapo Kikao cha mwisho cha uteuzi watia nia walioomba kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani hadi Julai 28 mwaka huu.

Taarifa ya Julai 20, 2025 kuhusu CCM

Ipo taarifa nyingine inayosambazwa katika mtandao wa Facebbok inayodai kuwa baadhi ya watia nia wa CCM tayari wamepitishwa na kamati kuu kugombea kwenye majimbo yao huku ikiweka orodha ya watia nia hao.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haijatolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Aidha muundo wa taarifa hiyo haufanani na taarifa rasmi ambazo hutolewa na CCM. Mathalani mpangilio wa sentensi haujaacha nafasi kwa kufuata mpangilio wa aya jambo linalodhihirisha kuwa ni taarifa ya kutengenezwa na wapotoshaji.

Kwa mujibu wa kiunganishi (Bar Code) kilichopo katika taarifa, kinathibitisha kuwa ni ya kughushiwa kutoka kwenye taarifa ya Juni 8, 2025, pia imetumia aina tofauti ya mwandiko (font) na unaotumiwa na chama hicho kwenye taarifa zao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma Julai 19, 2025 Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla alibainisha kuwa kikao cha mwisho cha uteuzi watia nia walioomba kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafanyika Julai 28 mwaka huu.

“Wagombea ni wengi, kazi kubwa imefanyika kwani tunataka haki itendeke kwa kufanya uteuzi makini, hivyo tumejipa nafasi mpaka tarehe 28."

“Wanachama na wagombea watulie, hakuna mtu aliyekatwa au kufyekwa. Tarehe 28 ndipo kutafanyika kikao cha mwisho cha uteuzi wa wagombea.”
​
Back
Top Bottom