Right Marker
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 194
- 625
Je, kwenye familia au ukoo wenu ulikutana na huu mkasa?
Wapo watu ambao wakizeeka hasa kuanzia umri wa miaka 70 na kuendelea, wanandugu mtapitia kipindi kigumu sana ambacho kama nyinyi hamtomuelewa mtaishia kugombana nyote, na hamtoelewana abadan.
Anaweza kuwa baba, mama, bibi, babu, dada, kaka, shangazi, mjomba, au mtu yeyote katika familia au ukoo wenu. Ingawa si wote ila wapo watu wa aina hiyo wakizeeka ni wasumbufu. Kila huduma nzuri mtakayompa kwake ni kero, na msipompa ni vita.
Kila siku ataamka na jambo jipya, kama si kuwachonganisha basi ni kuwavuruga mpaka vichwa vyenu vipate moto. Leo ataamka na hili, kesho na lile, kesho kutwa na hili, n.k
Ikiwa mnapitia changamoto hii kama ndugu hampaswi kugombana, bali mnapaswa kuelewa kwamba ndugu yenu mnayemtunza amezeeka, akili yake imerudi kuwa kama mtoto mdogo. Hivyo mnapaswa kuwa wamoja na kuzingatia lengo la kumtunza mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapompenda zaidi.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM