KERO Malipo ya likizo kwa Watumishi: Baadhi ya Halmashauri Mkoa wa Kigoma hawalipwi kulingana na Umbali

KERO Malipo ya likizo kwa Watumishi: Baadhi ya Halmashauri Mkoa wa Kigoma hawalipwi kulingana na Umbali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna Halmashauri iliyopo mkoa wa Kigoma, suala la malipo ya likizo haipewi kipaumbele na ukiomba malipo yanakatwa bila kupewa sababu ya msingi.

Unachoambiwa ni ujaze Vendor Form alafu unaingiziwa kiasi wanachojua wao.
Je! Kwanini elimu isitolewe kuhusu malipo ya likizo ili kuepusha kunyimwa haki ya Mtumishi?

Kuna muda wanasema uambatanishe Tiketi ya safari, na huku elimu haijatolewa kuhusu ticket za Digital.

Je! Tunapojaza taarifa kwa HR hazitoshi kuthibitisha ulipotokea?
 
upo anonymous na hata hiyo halmashauri unaificha utapata msaada kweli mkuu
 
upo anonymous na hata hiyo halmashauri unaificha utapata msaada kweli mkuu
Kwo mkuu unamaanisha, mhusika anaficha uchi halafu anataka kuzaa?

Sema, hii ni common sana kwa Waafrica... Sijui wasaidiweje
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Kwo mkuu unamaanisha, mhusika anaficha uchi halafu anataka kuzaa?

Sema, hii ni common sana kwa Waafrica... Sijui wasaidiweje
naam kama ni jambo la eneo kubwa alitakiwa kumwaga mchele
 
naam kama ni jambo la eneo kubwa alitakiwa kumwaga mchele
Sahihi. Aweke tatizo bayana litatuliwe. Vinginevyo itakuwa anataka kuzua taharuki na kusababisha migongano ya kimaslahi.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Sahihi. Aweke tatizo bayana litatuliwe. Vinginevyo itakuwa anataka kuzua taharuki na kusababisha migongano ya kimaslahi.
changamoto ya hizi anonymous ikishabandikwa ndo basi
 
Back
Top Bottom