A
Anonymous
Guest
Natokea Halmashauri ya Tanganyika Mkoa wa KATAVI, kuna tatizo kwenye malipo ya likizo kwa Watumishi wa Serikali, mfano likizo ya December 2024 kuna Watumishi hawajalipwa pesa hata mia, cha ajabu Mwaka 2025 walilipa kidogo.
Yaani kama unadai shilingi Laki 5 basi unalipwa laki moja, ila kuna Watumishi wengine majina yao hayakuonekana kwenye malipo na baada ya kufuatilia wakaambiwa wapeleke viambata vyao ili waweze kurekebishiwa.
Watumishi hao walipeleka ila juzi wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kabla hajaja kulitoka orodha ya majina wanaostahiki kulipwa likizo ya December 2024, ila wengi wao majina yao hayapo tena.
Kwa nini Mtumishi anapeleka viambata vya likizo halmashauri na wanavipokea, mara ya kwanza, wakati wa malipo jina halipo, Mtumishi huyo anaambiwa apeleke viambata tena.
Anapeleka wanavipokea, wakati wa malipo awamu ya pili jina halipo tena, je kosa la nani hapa? Kwa nini mtumishi asiambiwe mapema wakati anapeleka viambata vya likizo kuwa labda havijakidhi vigezo? Au wanalipana kwa kujuana?
Msaada unahitajika katika Halmashauri ya Tanganyika, watumishi wengi wanadai lakini hakuna msaada zaidi ya kuzungushwa tu.
Pia soma ~ Naibu Waziri Qwaray: Waajiri wote lazima watenge bajeti ya kumlipa mtumishi pindi anapohama