Baadhi ya watumishi wa umma Dar kufanyia kazi nyumbani Januari 27 na 28, 2025 sababu ya Mkutano wa Nishati Afrika

Baadhi ya watumishi wa umma Dar kufanyia kazi nyumbani Januari 27 na 28, 2025 sababu ya Mkutano wa Nishati Afrika

"Kufuatia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi kuwa tarehe 27 na 28 Januari, 2025 watumishi wa umma wa Mkoa wa Dar es Salaam wafanyie kazi nyumbani kutokana na barabara nyingi kufungwa ili kupisha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi barani Afrika, mnajulishwa kuwa wanafunzi wa shule na vyuo pia mnapaswa kusomea nyumbani kwa siku hizo mbili.

Taasisi na sekta binafsi mnashauriwa kufanya vivyo hivyo ili kupisha usumbufu ambao wafanyakazi na wanafunzi wanaweza kuupata." - Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali
 
Ufafanuzi hapa kwani wamesema ofisi za umma hata ambazo hazipo maeneo ya mkutano pia hakuna kwenda kazini? Kwa mfano kwa ambao wapo maeneo ya ubungo pia tangazo hili linawahusu
 
Back
Top Bottom