Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Waafrika ni shida kweli kweli. Kuna wakristo wanaojiona wao ni watakatifu kuliko hata Yesu mwenyewe aliyeleta huo ukristo.
Kama Yesu alikunywa mvinyo(kileo) inakuwaje wewe mfuasi wake useme kunywa pombe ni dhambi?
 
Ukatoliki pombe kitimoto sio dhambi infact wao wameamua kuzianzia hapa hapa duniani.

Hushangai ukobazini wao wameambiwa kuenjoy utamu wa kitimoto,pombe na kulombana wasubiri mpaka wafe huku jehanamu yao ni mwendo wa kuombana,kunywa kila aina ya pombe hadi mito itairirika pombe plus kitimoto kama kitoweo kikuu.

Mungu ibariki Israel
Uroho tu hata wasabato hawali kitimoto, huko peponi kitimoto pia haliwi yule, kulombana tunafanya hapa duniani na tutafanya tena huko peponi, kuhusu Pombe ndio tutakunywa peponi na itakuwa pombe saafi ambayo haina madhara wala kurukwa na akili kama hizi zenu mtu akinywa pombe anazeeka kabla ya muda na haja zina mtoka kama mtoto mdogo , halafu hao Waisrael wenyewe wenye dini yao ya uyahudi hawali kitimoto acha uroho
 
Hali ambayo wengi ninaozungumza nao wanajikuta wamo nayo ni hali ile ile ambayo mafarisayo na masadukayo walikuwa wanajisikia.

Wanaambiwa ukweli na wanaona huu ni ukweli kabisa.
Lakini hawawezi kamwe kuufata
Wamefungwa mpaka hawawezi kuufata,watafata kule wanaambiwa na kanisa na sio Mungu.

Tatizo ni nini??
DENOMINATIONAL SYSTEMS .

MIFUMO YA TANADUNI ILIYOWEKWA
Miaka na miaka wakatoliki wanakunywa pombe na kipi kinatokea? Wewe unayeamini kwamba unaweza kuibadllia dunia mwaka huu wa 2025 kwamba ndiye mwenye akili na wengine wote ni wajinga nadhani ndiye mwenye matatizo kuliko hao unaodhani wanatenda dhambi.

Walokole huwa mna matatizo ya akili, kudhani kwamba unaweza kwenda Ulaya bila ya visa bila ya passport kwa muujiza tu, kama wale sabato masalia walivyojidanganya mwaka 2008, ni ushahidi wa ugonjwa wa akili (delusional mindsets) sawa na yule mchungaji mwanamama kule Mwanza anayesema alishafika mbinguni akakutana na mitume pamoja na Yesu Mwenyewe!, hayo ni matatizo ya akili.

Dunia ipo kama ilivyo na hakuna kitu mnachoweza kufanya mkiamini eti mpo katika michakato ya kuibadilisha.
 
Kwahiyo tatizo liko wapi hapo?
Kila watu na imani zao. Hujaona kwenye makanisa mengi ya kikatoliki pembeni kunakua na nyumba ndogo za kuuza vyakula na vinywaji?
 
Yaan hapa aibu ni Kwa Gazeti alitoa taarifa au Kanisan??

Roman Catholic halijawahi kua Kanisa la kumfikisha mwanadamu katika Ufalme wa Baba Mungu .
Hapa duniani hakuna dini ya kukufikisha Kwenye ufalme wa Mungu. Imani yako ndio kitu pekee kitakusaidia.
 
Soma upya ufahamu maisha ya Yohana mbatizaji ndio utaelewa context ya hiyo habari.

Kwa kifupi sana, maisha ya Yohana mbatizaji yalikuwa yakujitenga na watu (akiishi Nyikani/porini) akiishi kwa kula nzige na asali, hii ilionekana kama sio kawaida kwa binadamu. Yesu alipokuja akaishi tofauti na Yohana, akikaa mijini zaidi, akijichanganya na watu zaidi kwenye tafrija mbalimbali, na hii ikatoa tafrisiri kuwa ni mlafi na mlevi.

Andiko hilo halihalarishi pombe, wala halisemi Yesu alikuwa mnywaji wa pombe, bali linatoa tafsiri ya maisha ya ujumla jumla ya Yohana vs Yesu.

Yesu hakutengeneza pombe kwakuwa divai ikitengenezwa papohapo haileweshi labda itunzwe kwa muda kidogo.(Ili fermentation itokee)
Na divai ikiwa tamu siyo kama ni kali inategemea na muda iliyohifadhiwa.
Search kitu kinaitwa "fermentation".
Hapa unajiona una elimu ya darasani ya kudadavua mambo kuliko padreeee 😃😃😃
 
Kwa hiyo kwako ni halali na vyema kanisa katoliki kuwaandalia waumini wake tafrija ya kunywa gongo nje ya jengo, lakini sio halali kuwaandalia ndani ya jengo la kanisa?
Kusema uongo ni dhambi iliyo katika amri kuu.. hapo sisi tunaona konyagi mwenzetu umeona gongo. Kwa imani ya kikristo kaungame usije enda motoni
 
W
Hata ibada zao zinatumia kiswahili tofauti
  1. Kitubio
  2. Mafungo
  3. Komunyio (kuna makabila hilo ni jina la sehemu ya mwili)
  4. Dominika
  5. Homilia
  6. Komunika
Ukiingia muumini mwingine unaweza kutoka kapa
Wewe unaona kiswahili ni tofauti, hilo jina lako unalotumia kuna maeneo ni tusi na pia kuna maeneo ni jina la mnyama au kitendo kibaya!
 
Back
Top Bottom