Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Waafrika ni shida kweli kweli. Kuna wakristo wanaojiona wao ni watakatifu kuliko hata Yesu mwenyewe aliyeleta huo ukristo.
Kama Yesu alikunywa mvinyo(kileo) inakuwaje wewe mfuasi wake useme kunywa pombe ni dhambi?
 
Uroho tu hata wasabato hawali kitimoto, huko peponi kitimoto pia haliwi yule, kulombana tunafanya hapa duniani na tutafanya tena huko peponi, kuhusu Pombe ndio tutakunywa peponi na itakuwa pombe saafi ambayo haina madhara wala kurukwa na akili kama hizi zenu mtu akinywa pombe anazeeka kabla ya muda na haja zina mtoka kama mtoto mdogo , halafu hao Waisrael wenyewe wenye dini yao ya uyahudi hawali kitimoto acha uroho
 
Miaka na miaka wakatoliki wanakunywa pombe na kipi kinatokea? Wewe unayeamini kwamba unaweza kuibadllia dunia mwaka huu wa 2025 kwamba ndiye mwenye akili na wengine wote ni wajinga nadhani ndiye mwenye matatizo kuliko hao unaodhani wanatenda dhambi.

Walokole huwa mna matatizo ya akili, kudhani kwamba unaweza kwenda Ulaya bila ya visa bila ya passport kwa muujiza tu, kama wale sabato masalia walivyojidanganya mwaka 2008, ni ushahidi wa ugonjwa wa akili (delusional mindsets) sawa na yule mchungaji mwanamama kule Mwanza anayesema alishafika mbinguni akakutana na mitume pamoja na Yesu Mwenyewe!, hayo ni matatizo ya akili.

Dunia ipo kama ilivyo na hakuna kitu mnachoweza kufanya mkiamini eti mpo katika michakato ya kuibadilisha.
 
Kwahiyo tatizo liko wapi hapo?
Kila watu na imani zao. Hujaona kwenye makanisa mengi ya kikatoliki pembeni kunakua na nyumba ndogo za kuuza vyakula na vinywaji?
 
Yaan hapa aibu ni Kwa Gazeti alitoa taarifa au Kanisan??

Roman Catholic halijawahi kua Kanisa la kumfikisha mwanadamu katika Ufalme wa Baba Mungu .
Hapa duniani hakuna dini ya kukufikisha Kwenye ufalme wa Mungu. Imani yako ndio kitu pekee kitakusaidia.
 

Yesu hakutengeneza pombe kwakuwa divai ikitengenezwa papohapo haileweshi labda itunzwe kwa muda kidogo.(Ili fermentation itokee)
Na divai ikiwa tamu siyo kama ni kali inategemea na muda iliyohifadhiwa.
Search kitu kinaitwa "fermentation".
Hapa unajiona una elimu ya darasani ya kudadavua mambo kuliko padreeee πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Kwa hiyo kwako ni halali na vyema kanisa katoliki kuwaandalia waumini wake tafrija ya kunywa gongo nje ya jengo, lakini sio halali kuwaandalia ndani ya jengo la kanisa?
Kusema uongo ni dhambi iliyo katika amri kuu.. hapo sisi tunaona konyagi mwenzetu umeona gongo. Kwa imani ya kikristo kaungame usije enda motoni
 
W
Hata ibada zao zinatumia kiswahili tofauti
  1. Kitubio
  2. Mafungo
  3. Komunyio (kuna makabila hilo ni jina la sehemu ya mwili)
  4. Dominika
  5. Homilia
  6. Komunika
Ukiingia muumini mwingine unaweza kutoka kapa
Wewe unaona kiswahili ni tofauti, hilo jina lako unalotumia kuna maeneo ni tusi na pia kuna maeneo ni jina la mnyama au kitendo kibaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…