Baadhi ya wavaa miwani mnakera sana

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Kuvaa miwani tunajua kuwa huenda una matatizo serious ya macho na sio urembo kwa baadhi ya watu wangine wafanyavyo

Lakini kuna kajitabia kanakofanywa na wavaa miwani kwa kweli kanakera sana,

Wakati unazungumza na mtu ambaye amevaa miwani badala ya kukuangalia kawaida na miwani yake, cha ajabu anakuangalia juu ya miwani

Yaani ameinamisha kichwa,macho yake yanakuangalia kwa kupenyeza juu ya miwani,inakera mno hii tabia halafu ni dharau kabisa,kama humuoni unayezungumza naye vizuri vua miwani mzungumze lakini sio kulazimisha macho yaangalie kwa kupitia juu ya miwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilichogundua bana hiyo ni auto-adapted behaviour kwa wavaa miwani wala si dharau.
ukitaka kuamini nunu miwan ha mwanga vaa wiki moja hakika utakuwa unawaangalia watu kama unavyo eleza.

[emoji375][emoji375]
 
Macho yangu kwa sasa hayahitaji miwani,hata nitakapovaa siwezi kumwangalia mtu kwa jinsi hiyo bora nivue

Sent using Jamii Forums mobile app
ungekuwa unatumia kompyuta mara nyingi au mda mrefu nina uhaakika sometime miwan ingekuwa inahusika.
nakuthibitishia ungetuangalia hivyo.
but just do as aconfirmatory test.

[emoji375][emoji375]
 
Hivi unajua aina za miwani ya macho ziko ngapi ?
Ngoja nikupe shule.
Miwani ya macho ipo ya aina mbili.
1.ya kuona karibu/ya kusomea maandishi madogo
2.ya kuona mbali.
Mara miwani ya kusomea/maandishi madogo ukimuangali mtu aliye umbali kidogo inakuwa humuoni vizuri ndo maana watu wengine huo wanaangalia kwa macho ya kawaida kupitia juu ya miwani.
Na siyo dharau au jeuri kama unavyofikiri
 
Lens ya miwani ni tofauti na natural lens ya jicho. Lens ya jicho zima, hubadilika vizuri saizi kulingana na umbali wa kitu kinachotizamwa. Ila lens ya miwani haina uwezo huo. Kama umevaa miwani ya kusomea, ukinyanyua kichwa na kutizama mbali, hutoweza kuona vizuri kwa sababu lens hiyo ni ya kuonea karibu na haibadiliki saizi unapotizama mbali. Ili uweze kuona mbali, inabidi usitumie lens ya miwani. Ndio hapo unamwona mwenye miwani akitumia kasehemu ka juu ya miwani kuona mbali vizuri. Siyo mikogo hiyo. Mungu akikupa umri, kuna siku utafika hatua hiyo na kuelewa vizuri.

 
Kuna bifocal lens mkuu inakusaidia kuona mbali na karibu.
 
Kuna bifocal inasaidia kunona mbali na karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…