Ushauti kuntu kabisa uliogusa angle zote. Msikilize huyu hapa.Wateja sio shida, biashara nyingi za kurithishwa utarithishwa mpaka wateja maana hapo kama umesimamia duka muda mrefu lazima una wateja wa kuanzia..
Kingine bishara sio cement pekee, unaweza ukawa na hardware na usiuze cement u focus na painting, nondo etc.
Kama una access ya cement unaweza pia ukafungua duka mtaji kidogo ukapelela kufyatua tofali au pavings block.
Kuna mdau hapo juu kasema Lori ni liability kwa kuanza lazima likupe stress Kama baba yako anafanya biashara zote lazima amekupa ambayo ameona utamudu msikilize usidhani hataki upate hizo faida unazoziona kichwani kwako
Ni rahisi kutoboa ukiwa na hardware moja kuliko fuso moja.Wana jamii mimi ni me 25 nakaa kwa wazazi nasimamia duka la jumla toka nimeanza kusimamia ni miaka 4 kwenda 5,
Sasa baba anataka kunifungulia duka la hardware hapa mjini ila nikiangalia maduka ya namna hiyo yapo mengi sana hapa mjini Kuna madogo ya kawaida na makubwa sana kama Kuna hili moja nimeskia jamaa kashika kiwanda kabisa cha cement kwahiyo najaribu kuangalia naona ni biashara yenye ushindani mkubwa sana
Hivo inaweza ikawa ngumu sana kupata wateja na kuaminika kwa haraka,mimi wazo langu nilitaka nilitaka huo mtaji atakao nipa aninunulie lory either fuso au Scania maana ni biashara ambayo na yeye pia anaifanya Ana malori nataka aninunulie ili niendelee kusimamia biashara zake mana na mm pia ni ndoto yangu kufanya biashara ya usafirishaji je ntakua nimefanya uamuzi sahihi.
Akishaelewa hichi tu basi atafanya maamuzi sahihi labda kama Baba yake atayahudumia magari yake😎Lori ni liability 100% wakati duka ni asset 100%