Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
Anaandika Baba Askofu Bagonza
MASUALA siyo MAJINA
Naendelea kuleta salaam za pole kwa watanzania wote. Poleni kwa msiba mzito. Faraja ya kweli itufunike sote.
Katika nyakati za kutafuta au kuchagua Viongozi, Baba wa Taifa alikuwa akisisitiza umuhimu wa kuchambua na kuorodhesha masuala kuliko kukimbilia kutaja majina. Alipenda masuala yanayoikabili nchi yazae majina ya wafaao kuongoza. Kutaja majina bila masuala huwaleta Viongozi wenye masuala yao mifukoni.
Naona watu wanakimbilia majina na sijaona anayejadili masuala. Kweli tuko msibani na kujadili majina bila masuala ni msiba mwingine.
Niliuanza mwaka huu kwa kupendekeza mradi mkubwa wa ujenzi wa umoja wa kitaifa. Hili ni suala KUU. Nionavyo Mimi masuala yafuatayo yatuongoze katika kufikia majina ya watakaomsaidia Rais Mteule:
1. Kiongozi asiyegawa watu ndani ya nchi na ndani ya chama chake (A non polarizing person).
2. Kiongozi anayekubali kushindwa, si kushinda kila wakati na kwa kila kitu.
3. Kiongozi asiye na matamanio ya nafasi ya urais, yaani amsaidie Rais bila kutamani kuwa Rais.
4. Kiongozi mwenye maono ya utawala bora kwanza ndani ya chama chake na ndani ya nchi.
5. Kiongozi asiyejaribiwa kutomshauri Rais juu upekee wa utawala wa sheria.
6. Kiongozi anayetamani Uhuru wa mihimili na kutafuta daima KUUONGEZA badala ya kuupunguza.
7. Kiongozi anayetamani kukubalika na kulindwa na umma.
8. Kiongozi anayethamini misingi ya demokrasia na maridhiano. Yule anayeona thamani ya wananchi kuwakilishwa katika vyombo vya maamuzi.
9. Kiongozi asiyetamani kubadilishana Uhuru na kitu chochote.
10. Kiongozi atakayeshauri njia bora za kulinda mazuri ya Rais Magufuli na jasiri mwenye upendo wa kukosoa na kurekebisha yaliyo na upungufu.
11. Kiongozi asiyejisikia dhaifu kuridhika na kuongoza maridhiano ya kitaifa.
12. Kiongozi anayemshauri Rais juu ya ULAZIMA wa kujenga na kuimarisha taasisi imara na kukatisha tamaa ujenzi wa nafsi imara katika taasisi.
13. Kiongozi atakayemshauri Rais uimarishaji wa uchumi wa watu binafsi bila kudhoofisha uchumi wa dola.
Sifa hizi na masuala haya, vituzalie majina. Msiba wa Baba/Mama wa familia hunoga pale anapopatikana mrithi atoshaye na kufariji waombolezaji.
Mama Samia Suluhu Hassan unapolia, pangusa machozi upesi na kuangaza macho yako kumwona atoshaye kushughulikia masuala haya. Usikalishe leso muda mrefu machoni ili wazuri wasije kupita mbele yako bila kuwaona.
APUMZIKE KWA AMANI JPM.