Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Tuna mambo mengi na muda mchache au mfupi wa kuyasikiliza. Mzee Butiku kamaliza kusema. Kapingwa na kupuuzwa. Lakini tujiulize: Saa mbovu ikisema muda sahihi tutaitii na kuamka au tutapuuza? Mzee Butiku anaweza kuwa katumwa au kachanganywa na wale jamaa LAKINI jambo moja kapatia. HATUKO SAWA na TUNA TATIZO. Shetani aletaye habari njema ni bora kuliko malaika aletaye habari mbaya. Natafakari:
1. Mtu mzito (Kigogo kweli), kaniita. Kasema “tatizo ni namba 1 na 2 hawapatani lakini namba 2 hana hela tumemkimbia. Hana lolote yule. Siasa za umaskini aliondoka nazo Kambarange. Huyu ni Yuda tu kamsaliti mwenzake”
Nikamwuliza: Fedha zimeanza lini kuwa kigezo cha uongozi? Akakata simu. Wanaopenda fedha hawapendi kuulizwa maswali magumu.
2. Kaniita mwingine. Huyu ni Kada wa chama chetu kilichogeuka chao. Akasema, “hata uchaguzi ukirudiwa tutashinda. Tuna hela za kutosha kununua uchaguzi mpaka 2035. Hakuna asiye na bei nchi hii. Hata wewe tunakulia timing”. Nikamwuliza hata huu uchaguzi unaobishaniwa mliununua? Akajibu kwa kifupi akasema, “Kumbe wewe hujui!?”
Nikatoa kilio, Wewe fedha umelaaniwa ndiyo maana ulimuuza Yesu.
3. Akapiga askari asiyevaa kombati isipokuwa suti. Anatoka lile “jeshi la malaika wa duniani”. Nililiamini jeshi hili mpaka nikajisahau. Akasema, “ Mkononi tuna chuma na mkwanja. Mtu achague moja. Apokee mkwanja mambo yaishe au akatae ale chuma.” Nikabaki mdomo wazi.
Zamani zetu askari wa jeshi la malaika hawa angeweza kukaa na sanduku la hela za KAZI MAALUMU”, lakini akaenda duka la Mangi kukopa chumvi. Nini kimetokea? Fedha zimeharibu; si Mabeberu.
4. Akaja Mbunge na Waziri Mstaafu. Akasema, “Fedha ni kila kitu. Ni rahisi kumhonga mbunge apitishe sheria au bajeti kuliko kumhonga Karani wa ofisi akuibie document. Lunch ya Ikulu na semina moja yenye posho kubwa inatosha kumlainisha. Mbunge aliyeshindikana anapewa safari moja ya nje, akirudi anagonga meza mpaka inatoboka”.
Hatuhitaji mabeberu kulivuruga bunge. Fedha inatosha na ina nguvu kuliko bunge lenyewe. Chanjo ya uzalendo kwa wabunge itoke wapi?
5. Akamalizia Mnikulu wa awamu ya 4:
Akasema, “tuna ombwe (vaccum). Tiketi haielewani. Mmoja yuko tayari yaishe lakini waondoke wote ili kuunganisha taifa. Mwingine hataki, na hela hataki. Tunajiandaa kurudi kuliokoa taifa. Hatutagusa vyombo vyetu.”
Mpaka hapa, Nani asiyeona haja ya Maridhiano? Wengi tunayataka. Tunachoogopa ni HILA.
Hila zinachelewesha maridhiano.
Katika awamu ya pili, Baba wa Taifa aliandika maneno haya: “Majuto ni mjukuu, huja baadaye. Tunaweza kufikishwa mahali tukiulinganisha uongozi wa Rais Mwinyi na wa Rais wa kesho tukaona kuwa chini ya Ndugu Mwinyi, pamoja na udhaifu wake wote, tulikuwa peponi” (ukurasa 52, UONGOZI WETU..).
SIKILIZA: Enzi zisizo hizi:
-Tutalazimika kukaa meza moja
kuridhiana na wana harakati (Rachel
Dangwa, Mange Kimambi, Mjaluo
Maria Sarungi, nk). Bora turidhiane
kabla hatujafika huko. Tuache
kigugumizi. Tukiri kosa, tusonge
mbele. Ubishi wa Mjaluo haumfanyi
kuwa Mkurya.
Ukiona dalili hizi; jifunze kuweka akiba ya maneno. Chukia fedha, jifunze kujenga hoja. Rudisha silaha ghalani na upanga alani. Fungulia wafungwa na bomoa mahabusu tukose pa kukufungia wewe yakikukuta. Hakuna umilele wa ufalme wa dunia.
Wajaluo wanasema: “Maskini akitabiri ujio wa nzige, huzodolewa kuwa ana hamu ya kuwala”.

- Mpagani atazaa muumini.
- Asiyejua, atajua.
- Msomi atazaa mjinga