Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Jimbo la Arusha Mjini, Emanuel Zakaria maarufu kama Baba Bony, ametoa onyo kali kwa kundi la G- 55 ambalo linapinga msimamo rasmi wa chama hicho wa "No Reforms, No Election" kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akizungumza mara baada ya tamko la aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, Baba Bony amesema hatua ya kundi hilo ni sawa na kutaka kuligawa chama na kudhoofisha harakati za kuleta mageuzi ya kweli katika mfumo wa uchaguzi nchini.
Aidha, ametoa wito kwa uongozi wa CHADEMA kuvunja makundi yote yaliyotokana na uchaguzi wa ndani wa chama na kuhoji chanzo cha kundi hilo:
Kauli ya Baba Bony imekuja wakati ambapo hali ya joto la kisiasa ndani ya CHADEMA inazidi kupanda, huku mjadala mkali ukitawala mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya kisiasa kuhusu iwapo chama hicho kisusie uchaguzi mkuu iwapo marekebisho ya msingi hayatafanyika.