Baba Chaula: Nimepigiwa simu na namba ngeni, kaniambia nitoe Tsh. Milioni 3 ili Chaula apatikane

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Screenshot 2024-08-31 153842.png

Mzee Yusuph Sisala Chaula akiwa na mwanaye Shadrack Chaula

Kufuatia taarifa za kupotea katika mazingira yanayodaiwa ‘kutekwa’ kwa Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, baba mzazi wa kijana huyo, mzee Yusuph Sisala Chaula amesema amepigiwa simu akitakiwa kutoa Shilingi Milioni 3 ili aweze kumpata mwanaye.

Mzee Chaula anasema “Nimepigiwa simu na namba ambayo siifahamu, namba yenyewe ni 0763 55.... na wala mhusika hakujitambulisha, ameniambia natakiwa kukubali kutoa Shilingi milioni tatu ili niweze kumpata mtoto wangu.

“Nikamwambia sawa kama ni mzima na yuko salama sawa ngoja tutafute hiyo fedha. Baada ya kujadiliana na familia tukaona bora tutoe hiyo taarifa Polisi kwa kuwa wao ndio wanaohusika na upelelezi.
1722618599819.png

Shadrack Chaula
“Nimetoa taarifa na kuikabidhi namba husika kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kiwila pamoja na kwa mpelelezi wa suala hilo la kupotea kwa mtoto wangu katika mazingira ya kutatanisha.

“Simu hiyo nilipigiwa mchana wa Agosti 30, 2024 na hadi sasa Agosti 31 bado sijapata mrejesho wowote kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu hiyo namba au huyo mtu aliyepiga, pia sijajulisha mpaka sasa upelelezi wa Shadrack umefikia wapi.”

JamiiForums ilipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga kuhusu suala hilo amesema “Bado sijapata taarifa kuhusu suala hio, nipo kwenye mbio za Mwenge, labda nikirejea nitapata taarifa.”

Pia soma:
~ Baba Chaula: Polisi niambieni mwanangu kama yu hai tu basi inatosha, nahisi roho yangu inashindwa kuvumilia haya maumivu

~ Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo
 
Kufuatia taarifa za kupotea katika mazingira yanayodaiwa ‘kutekwa’ kwa Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, baba mzazi wa kijana huyo, mzee Yusuph Sisala Chaula amesema amepigiwa simu akitakiwa kutoa Shilingi milioni 3 ili aweze kumpata mwanaye.

Mzee Chaula anasema “Nimepigiwa simu nan amba ambayo siifahamu, wala mhusika hakujitambulisha, ameniambia natakiwa kukubali kutoa Shilingi milioni tatu ili niweze kumpata mtoto wangu.

“Nikamwambia sawa kama ni mzima na yuko salama sawa ngoja tutafute hiyo fedha. Baada ya kujadiliana na familia tukaona bora tutoe hiyo taarifa Polisi kwa kuwa wao ndio wanaohusika na upelelezi.

“Nimetoa taarifa na kuikabidhi namba husika kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kiwila pamoja na kwa mpelelezi wa suala hilo la kupotea kwa mtoto wangu katika mazingira ya kutatanisha.

“Simu hiyo nilipigiwa mchana wa Agosti 30, 2024 na hadi sasa Agosti 31 bado sijapata mrejesho wowote kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu hiyo namba au huyo mtu aliyepiga, pia sijajulisha mpaka sasa upelelezi wa Shadrack umefikia wapi.”

JamiiForums ilipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga kuhusu suala hilo amesema “Bado sijapata taarifa kuhusu suala hio, nipo kwenye mbio za Mwenge, labda nikirejea nitapata taarifa.”
Kama walichanga mil 7 kwa mhuni mzee nenda pale kwenye kile chama lia watakuchangia fasta...
 
JamiiForums ilipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga kuhusu suala hilo amesema “Bado sijapata taarifa kuhusu suala hio, nipo kwenye mbio za Mwenge, labda nikirejea nitapata taarifa.”
Ndiyo sisi hao, inachukua muda gani kupiga simu na kutoa majibu, anaona kuwa kwenye mbio za mwenge ni sifa
 
View attachment 3083542
Mzee Yusuph Sisala Chaula akiwa na mwanaye Shadrack Chaula

Kufuatia taarifa za kupotea katika mazingira yanayodaiwa ‘kutekwa’ kwa Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, baba mzazi wa kijana huyo, mzee Yusuph Sisala Chaula amesema amepigiwa simu akitakiwa kutoa Shilingi Milioni 3 ili aweze kumpata mwanaye.

Mzee Chaula anasema “Nimepigiwa simu na namba ambayo siifahamu, namba yenyewe ni 0763 55.... na wala mhusika hakujitambulisha, ameniambia natakiwa kukubali kutoa Shilingi milioni tatu ili niweze kumpata mtoto wangu.

“Nikamwambia sawa kama ni mzima na yuko salama sawa ngoja tutafute hiyo fedha. Baada ya kujadiliana na familia tukaona bora tutoe hiyo taarifa Polisi kwa kuwa wao ndio wanaohusika na upelelezi.
View attachment 3083527
Shadrack Chaula
“Nimetoa taarifa na kuikabidhi namba husika kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kiwila pamoja na kwa mpelelezi wa suala hilo la kupotea kwa mtoto wangu katika mazingira ya kutatanisha.

“Simu hiyo nilipigiwa mchana wa Agosti 30, 2024 na hadi sasa Agosti 31 bado sijapata mrejesho wowote kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu hiyo namba au huyo mtu aliyepiga, pia sijajulisha mpaka sasa upelelezi wa Shadrack umefikia wapi.”

JamiiForums ilipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga kuhusu suala hilo amesema “Bado sijapata taarifa kuhusu suala hio, nipo kwenye mbio za Mwenge, labda nikirejea nitapata taarifa.”

Pia soma:
~ Baba Chaula: Polisi niambieni mwanangu kama yu hai tu basi inatosha, nahisi roho yangu inashindwa kuvumilia haya maumivu

~ Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo
Sasa kama watekaji wako humu,si tayari wesha jua kua mzee kesha peleka taarifa za milioni 3 police!? Kuna vitu vingine si vya kutangaza haraka haraka kabla ya uchunguzi wa kina!!
 
Mnaweza laumu serikali lakini kumbe ni lack of exposure and awareness yao ni ndogo.

Biashara za kuteka watu hela zipo,
Biashara za kukodi wauaji zipo,

Sema ukute viongozi wanashupaza vichwa mana hawajui hilo huku wakiona lawama wanapewa wao.
 
View attachment 3083542
Mzee Yusuph Sisala Chaula akiwa na mwanaye Shadrack Chaula

Kufuatia taarifa za kupotea katika mazingira yanayodaiwa ‘kutekwa’ kwa Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, baba mzazi wa kijana huyo, mzee Yusuph Sisala Chaula amesema amepigiwa simu akitakiwa kutoa Shilingi Milioni 3 ili aweze kumpata mwanaye.

Mzee Chaula anasema “Nimepigiwa simu na namba ambayo siifahamu, namba yenyewe ni 0763 55.... na wala mhusika hakujitambulisha, ameniambia natakiwa kukubali kutoa Shilingi milioni tatu ili niweze kumpata mtoto wangu.

“Nikamwambia sawa kama ni mzima na yuko salama sawa ngoja tutafute hiyo fedha. Baada ya kujadiliana na familia tukaona bora tutoe hiyo taarifa Polisi kwa kuwa wao ndio wanaohusika na upelelezi.
View attachment 3083527
Shadrack Chaula
“Nimetoa taarifa na kuikabidhi namba husika kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kiwila pamoja na kwa mpelelezi wa suala hilo la kupotea kwa mtoto wangu katika mazingira ya kutatanisha.

“Simu hiyo nilipigiwa mchana wa Agosti 30, 2024 na hadi sasa Agosti 31 bado sijapata mrejesho wowote kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu hiyo namba au huyo mtu aliyepiga, pia sijajulisha mpaka sasa upelelezi wa Shadrack umefikia wapi.”

JamiiForums ilipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga kuhusu suala hilo amesema “Bado sijapata taarifa kuhusu suala hio, nipo kwenye mbio za Mwenge, labda nikirejea nitapata taarifa.”

Pia soma:
~ Baba Chaula: Polisi niambieni mwanangu kama yu hai tu basi inatosha, nahisi roho yangu inashindwa kuvumilia haya maumivu

~ Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo
hao ni matapeli, mtoto yuko na polisi! Amuachie Mungu atatoa suluhisho!
 
Back
Top Bottom