Baba Chaula: Nimepigiwa simu na namba ngeni, kaniambia nitoe Tsh. Milioni 3 ili Chaula apatikane

Mnaweza laumu serikali lakini kumbe ni lack of exposure and awareness yao ni ndogo.

Biashara za kuteka watu hela zipo,
Biashara za kukodi wauaji zipo,

Sema ukute viongozi wanashupaza vichwa mana hawajui hilo huku wakiona lawama wanapewa wao.
Kwa hiyo madai ya Mbowe kuhusu Polisi kuhusika kwa kuwataja majina wahusika ni madai ya uongo?

Mambo yote uliyoyaongea yapo katika jamii, lakini madai ya vyombo vya dola vinavyohusika na ulinzi wa roho za raia, kwetu sisi ndiyo habari kubwa kuliko hizi zinazozushwa sasa hivi kufunika uovu wa vyombo vya Serikali.

Ungelitaka ueleweke vizuri ungeanza kulaani kwanza Polisi watekaji, ndiyo uje sasa na hoja ya mahaba na 'gavumenti' yako na tena uijengee hoja ya utetezi yenye akili, maana raia wengi Tz kwa sasa, washazielewa mbivu na mbichi, waweza usieleweke.
 
hao ni matapeli, mtoto yuko na polisi! Amuachie Mungu atatoa suluhisho!
Pia kuna uwezekano watekaji wake ambao wanaweza kuwa ni hao watekaji wenye namba halali vifuani mwao ili kuwapoteza maboya wananchi wakaandaa watu wa kuwapigia simu wazazi kudai pesa ili kujenga mazingira kuwa kijana alitekwa na watu wenye nia ya kujipatia pesa na siyo wao.
 
Ukijiona kwenu maisha ya kuungaunga usijiingize kwenye masuala ya uwanaharakati wa vyama vya siasa.

Unapomtukana Rais ina maana umeitukana system nzima ya nchi.

Vijana kuweni makini mdomo uliponza kichwa. Mwenye mamlaka kashika mpini ,wewe raia umeshika makali. Ukimkosoa au kushamshauri tumia lugha za kistaarabu na kiungwana. Laa sivyo itakayoteseka ni familia yako
 
Watu waisome hii na waielewe. Kiafrica mfumo unaweza kukufanya lolote na familia isiwe na pa kusemea zaidi ya maumivu kuwaachia. Mimi hizi habari za siasa sijui kupiga kura sina mda nazo'
 
Awe makini tu, wasije kuna watu wakawa wanataka kupiga hela tu na watokomee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…