Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kufuatia taarifa za kupotea katika mazingira yanayodaiwa ‘kutekwa’ kwa Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, baba mzazi wa kijana huyo, mzee Yusuph Sisala Chaula amesema anaomba ajulishwe tu mwanaye kama yu hai au la ili moyo wake uwe na amani.
Amesema “Unajua inaweza kufa roho moja lakini hiyo moja ikafa na nyingine kadhaa kutokana na mawazo. Siku ya nne sasa sijui mwanangu yuko wapi.
“Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi lakini mpaka sasa wapo kimya na sina taarifa zozote, kama yupo hai waniambie tu ili nafsi yangu itulie, kama ameshikiliwa na Vyombo vya Usalama waniambie tu pia nijue yupo hai tutaenda kumuona.
“Hata kama yupo gerezani waniambie tu nitajua yupo hai na ipo siku nitaenda kumuona, naongea kwa uchungu sana, najiona nashindwa kuvumilia haya maumivu, sijui nini kitatokea, lakini naomba Serikali iniambie tu mwanangu yuko hai hata kama wanaendelea kumshikilia kuliko huu ukimya uliopo sasa.
“Mara ya mwisho tumewasiliana na Mpelekezi tuliyepewa asimamie suala hilo jana (Agosti 5, 2024) baada ya hapo hatujapata taarifa nyingine ya ziada.”
JamiiForums ilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, jana Agosti 5, 2024, alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema “Nipo msibani tutawasiliana baadaye.” Baada ya hapo simu yake haikupokelewa.
Alipotafutwa leo Agosti 6, 2024, simu haikupokelewa, akatuma ujumbe “Nitakupigia baadaye.”
Ikumbukwe Julai 8, 2024, Shadrack Chaula aliachiwa huru kutoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 ikiwa ni siku chache tangu kuhukumiwa kifungo cha Miaka Miwili jela au kulipa Faini hiyo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo Mtandaoni.